Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yatinga nusu fainali FA ikiichapa Mbeya City

Muktasari:

  • Baada ya kutinga katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba imeendelea kufanya vizuri ikifuzu tena hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB.

Dar es Salaam. Simba imetinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo uliochezwa leo Jumapili, Aprili 13, 2025 kwenye uwanja wa KMC, Complex Dar es Salaam.

Simba ilitoka nyuma kwa bao moja baada ya Mbeya City kuanza kufunga bao  kupitia kwa mshambuliaji Mudathir Said katika dakika ya 22 huku bao la kusawazisha la Simba likifungwa katika dakika ya 24 na Fabrice Ngoma.

Dakika ya 29, Leonel Ateba aliifungia Simba bao la pili akimalizia kichwa mpira wa krosi uliochongwa na Fabrice Ngoma huku bao la tatu likifungwa na Joshua Mutale katika dakika ya 43.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Simba ilikuwa mbele kwa mabao 3-1

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kumiliki mpira kwa asilimia kubwa huku ikilishambulia mara kwa mara lango la Mbeya City na hadi dakika 90 zinamalizika Wekundu wa Msimbazi walilinda ushindi wao walioupata kipindi cha kwanza.

Licha ya kufunga bao moja kwenye mchezo wa leo mshambuliaji wa Simba, Leonel Ateba bado ameonekana kukosa utulivu wakati wa kushambulia kwani ameshindwa kuzitumia nafasi kadhaa za wazi alizopata.

Baada ya kusonga katika hatua ya nusu fainali, Simba inatarajia kukutana na mpinzani kati ya Singida Black Stars au Kagera Sugar ambazo zitavaana kesho kwenye uwanja wa Liti, mkoani Singida.