Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaichapa Namungo, ikigeukia Kombe la Muungano

Beki wa kushoto wa Simba, Antony Mligo wakati akijaribu kumzuia mchezaji wa Namungo katika mechi ya Ligi Kuu iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 3-1 katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa. Picha na Simba

Muktasari:

  • Katika mechi 14 ambazo Namungo na Simba zimekutana kwenye Ligi Kuu, Simba imeibuka na ushindi mara tisa na matokeo ya sare ni mara tano.

Dar es Salaam. Simba imezidi kujichimbia katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya leo, Jumapili, Aprili 19, 2026 kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Namungo FC katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi.

Ikiingia na historia nzuri ya ubabe dhidi ya Namungo FC kwa kutowahi kupoteza mechi hata moja ya Ligi Kuu dhidi yao, Simba ilionyesha mapema dalili za kuibuka na ushindi katika mechi hiyo kwa kwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1.

Libasse Gueye ndiye amefunga bao la kwanza la Simba katika dakika ya 12 akimalizia pasi ya Anthony Mligo na dakika 13 baadaye Anicet Oura akawafungia bao la pili akimalizia pasi ya Yusuph Kagoma.

Dakika ya 33, Namungo walipachika bao lao la kufutia machozi katika mechi hiyo kupitia kwa Heritier Makambo kwa mkwaju wa penalti iliyotokana na Kagoma kunawa mpira katika eneo la hatari.

Kipindi cha pili, Simba ikajihakikishia ushindi kupitia bao la Elie Mpanzu katika dakika ya 74.

Matokeo hayo yameifanya Simba iendelee kubakia katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikifikisha pointi 42.

Ushindi huo pia umeifanya Simba iendeleze ubabe wake dhidi ya Namungo FC kwenye Ligi Kuu ya NBC ambapo hadi sasa haijapoteza mechi dhidi yao.

Katika mechi hizo 14 zilizowahi kuzikutanisha, Simba imeibuka na ushindi mara tisa na zimetoka sare tano.