Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba bado yamwania kiungo CS Sfaxien

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Kama Simba itamchukua kiungo huyo itabidi mchezaji mmoja wa kigeni atolewe kwenye hesabu za kikosi hicho ili nafasi hiyo ipatikane.

Mabosi wa Simba bado wamemganda, kiungo wa CS Sfaxien ya Tunisia, Balla Moussa Conte baada ya kufanya naye mazungumzo na kwa sasa wanasikilizia uamuzi wa mwisho wa klabu anayoichezea ili atue Msimbazi kwa msimu ujao.

Simba ilimuona kiungo huyo katika mechi dhidi ya kikosi hicho hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, ilipowachapa Kwa Mkapa kwa mabao 2-1 kisha kwenda kuifunga kwao  1-0.

Hata hivyo Mwananchi inafahamu, dili hilo liliishia njia katika dirisha dogo licha ya mazungumzo ya mwisho mchezaji aliwaambia wampe pesa ili asitishe mkataba alionao Sfaxien.

Taarifa za ndani zinasema, Simba ilikubaliana na Conte kwamba, mwishoni mwa msimu watampatia pesa ambazo wamekubaliana ili aweze kuuza mkataba wake na hivi karibuni walirudi kukumbushia.

"Ili kiungo huyo atue ndani ya Simba inabidi amalize mkataba au auvunje, jambo ambalo hawezi kulifanya kama hatopewa pesa na Wekundu hao."

Hapo awali kupitia Mwananchi iliandika kuwa; Mara ya kwanza Fadlu alivutiwa na uwezo wa kiungo huyo katika mchezo uliopigwa hapa Dar Desemba 15, 2024 ambapo Simba ilishinda 2-1 huku Conte akikichafua dakika zote tisini.

“Baada ya mchezo wa kwanza, Fadlu akataka kujidhihirisha zaidi mchezo wa pili ambapo pia kiungo huyo alicheza dakika zote tisini kwa kiwango kizuri sana.”

Chanzo hicho kilisema kuwa, baada ya mchezo huo wa pili uliochezwa Tunisia, Fadlu alimpa jukumu kipa wake, Moussa Camara kwenda kuzungumza na Conte ambaye anatoka naye nchi moja ya Guinea.


CONTE NI NANI?

Ni kiungo wa ukabaji mzaliwa wa Kamsar, Guinea ana uwezo pia wa kucheza nafasi ya kiungo cha ushambuliaji.

Kiungo huyo aliyezaliwa Aprili 15, 2004 na amekuwa mhimili mzuri ndani ya CS Sfaixien alichojiunga nacho Februari Mosi, 2023, huku malezi yake ya soka akiyapata katika Kituo cha Academie La Louvia kilichopo kwao Guinea.

Katika kikosi cha CS Sfaxien chenye mchanganyiko wa wachezaji wa mataifa mbalimbali ikiwemo Mali, Algeria, Tunisia, Guinea na Ivory Coast, kiungo huyo ni nyota wa tano kati ya wenye thamani kubwa klabuni hapo.

Katika listi ya wachezaji wa CS Sfaxien wenye thamani kubwa, anaanza Mohamed Nasraoui (bilioni 1.8) sawa na Hichem Baccar na Mohamed Dhaoui ‘Cristo’. Anayefuatia ni Aymen Dahmen (bilioni 1.7) kisha ndiyo Balla Moussa Conte (bilioni 1.4).

Licha ya kwamba Simba, tayari kuna viungo wakabaji watatu wa kimataifa ambao ni Fabrice Ngoma, Debora Mavambo na Augustine Okejepha, mbali na wazawa, Yusuf Kagoma na Mzamiru Yassin, lakini kochaFadlu Davids anamhitaji nyota huyo wa Sfaxien ili kuongeza ushindani na kuna atakayeng'olewa.

Kati ya nyota hao, Ngoma ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika Juni 30, 2025, ameonekana kuwaka sana kiasi cha kuhatarisha nafasi za wenzake waliojiunga mwanzoni mwa msimu huu, huku yeye akiandaliwa mkataba mpya.

Kama Simba itamchukua kiungo huyo itabidi mchezaji mmoja wa kigeni atolewe kwenye hesabu za kikosi hicho ili nafasi hiyo ipatikane.

Conte mwenye umri wa miaka 20 anatakiwa na Fadlu katika kufanikisha projekti yake ya muda mrefu kuijenga timu hiyo, kwani tangu ametua Julai 2024, asilimia kubwa ya wachezaji aliowasajili ni chini ya miaka 25, hivyo kiungo huyo ni mtu sahihi kwake kwa faida ya baadaye.