Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siku tisa za presha, heshima

Muktasari:

  • Baada ya kumaliza mechi za Ligi Juni 15 siku tatu mbele Yanga itakabiliana na Singida Black Stars katika mechi ya fainali ya FA ili kuhakikisha inatetea kombe lake lingine.

Zimebaki siku tisa tu kabla bingwa wa Ligi Kuu Bara hajapatikana, ukiwa ni ubingwa ambao unaushindani mkubwa zaidi kwa misimu kadhaa ya hivi karibuni.

Timu za Yanga na Simba ndizo zinawania ubingwa msimu huu, sasa zikiwa zimebaki mechi tatu tu dhidi yao na Yanga ipo mbele ya Simba kwa tofauti ya pointi moja, yeyewe ina pointi 73 huku Simba ikiwa na pointi 72 zote zimecheza michezo sawa.

Kwa upande wa Simba presha ni kubwa zaidi kwa kuwa ina ifanikiwe kutwaa ubingwa ni lazima iombe mambo mawili yaweze kutokea.

Moja Simba inatakiwa kuhakikisha inashinda michezo yake yote mitatu dhidi ya KenGod Juni 18, Kagera Sugar Juni 22 pamoja na ule wa dabi ya Kariakoo Juni 25.

Pili, iombe Yanga idondoshe pointi kwenye michezo yake miwili, dhidi ya Prisons Juni 18 ambao unaonekana kuwa mchezo mgumu kwa kuwa Maafande hao wapo kwenye hatari ya kucheza mechi za mtoano 'play off' pamoja na ule dhidi ya Dodoma, Juni 22.

Lakini kama mambo yataenda kama yalivyo, Yanga inaweza kuingia kwenye mchezo wa dabi ikiwa na faida ya mambo mawili, inaweza kupata sare na kutwaa ubingwa kwa kuwa hadi sasa ipo juu ya Simba kwa pointi moja lakini pia ikiwa na mabao manane zaidi.

Lakini presha ya pili kwa Simba inafahamika kwa sasa inawania taji moja pekee la ligi baada ya kuondolewa kwenye Kombe la FA lakini pia kushindwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika ilipochapwa na Berkane mabao 3-1 kwenye fainali lakini watani zao wa jadi wanayo mawili wakipambana kuyatetea.

Yanga imeingia fainali ya Kombe la FA ikienda kucheza dhidi ya Singida Black Stars, Juni 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, lakini pia kabati kwa mabingwa hao wa kihistoria wana Kombe la Muungano pamoja Ngao ya Jamii mbayo wamechukua msimu huu.

Baada ya kumaliza mechi za Ligi Juni 15 siku tatu mbele Yanga itakabiliana na Singida Black Stars katika mechi ya fainali ya FA ili kuhakikisha inatetea kombe lake lingine.

Hii ina maana kuwa Yanga sasa ina siku 11 kubakiza heshima yake ya makombe mawili ambayo ilitwaa msimu ulioipita, huku Simba ikiwa na siku tisa za kuweka heshima mpya.

Hata hivyo, ukiachana na mchezo wa Dabi ya Kariakoo, Simba inaonekana kuwa na mteremko kwenye michezo yake, KenGold tayari imeshashuka daraja pamoja na Kagera Sugar, huku Yanga ugumu ukionekana kwenye mchezo dhidi ya Prisons pekee kwa kuwa ipo kwenye wakati mgumu, huku Dodoma Jiji ikiwa salama kwenye Ligi baada ya kukusanya pointi 34 ikiwa nafasi ya saba.


Makocha wawajipanga

Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi amesema: “Tuna jukumu la kutetea ubingwa wa ligi, hiki ni kitu ambacho hakiepukiki, tunajituma ili kuhakikisha ubingwa huu tunaendelea kuushikilia, nafahamu ligi ni ngumu lakini kama Yanga hatutakiwi kuogopa kwa kuwa nia na ubora wa kufanya hayo tunao, tutafanya kila linalowezekana kuchukua ubingwa huu na ule wa Kombe la FA.

Kwa upande wa kocha wa Simba SC, Fadlu Davids, amesema: "Tuna mechi ambazo kwetu ni kama fainali. Hatuwezi kujiamini sana wala kuangalia wapinzani wetu wanavyofanya. Tunapaswa kuhakikisha tunashinda kila mchezo. Hakuna nafasi ya kupumzika."


Ratiba ya ubingwa

Prisons vs Yanga

Yanga vs Dodoma

Yanga vs Simba

KenGold vs Simba

Simba vs Kagera

Yanga vs Simba