Sikia Gerrad alichomshauri Salah sakata lake na Slot
Muktasari:
- Salah alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu England msimu uliopita akiifungia Liverpool mabao 29.
Gwiji wa Liverpool Steven Gerrard ametoa mawazo yake juu ya mgogoro unaoendelea dhidi ya Mohamed Salah akidai klabu hiyo 'inamhitaji tena' mshambuliaji huyo.
Salah aliibua sintofahamu Jumamosi jioni alipotoa maneno makali dhidi ya Liverpool na Meneja wake Arne Slot katika uwanja wa Elland Road ambako timu yake ya Liverpool ilitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Leeds United.
Mshambuliaji huyo Raia wa Misri ambaye ambaye hakutumika usiku huo, alidai kuwa 'alitupwa chini ya basi' na Liverpool huku kukiwa na kiwango kisichoridhisha na baadaye aliondolewa kwenye kikosi cha Arne Slot cha Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter MInter Milan Jumanne.
Kauli hiyo ya Salah imeleta wimbi la ukosoaji kwa kwake huku Jamie Carragher akiitaja kuwa 'fedheha'. Na sasa, Gerrard amekiri Salah alikosea kuwasilisha malalamishi yake hadharani.
'Ni wazi amekasirika sana kutocheza, jambo ambalo naheshimu. Ni wazi anataka kusaidia timu, ambayo ninaiheshimu.
'Mistari michache kuhusu kutupa watu chini ya basi, si sawa. Kuna haja ya kugeuka mbali kidogo na hiyo ili kukabiliana na hilo na meneja. Hili linahitaji Virgil van Dijk aende, "Tunatatuaje hili?" Hata si kwa manufaa ya klabu, au timu, ni mashabiki," amesema Gerrard.
Wakati Gerrard akisema hayo, Slot amesema kuwa yuko tayari kumaliza mgogoro huo lakini iwapo Salah atafanya mambo mawili.
Akizungumza baada ya mechi dhidi ya Inter Milan, Slot amemtaka Salah kwanza afahamu kwamba amekosea na jambo la pili ni mchezaji mwenyewe kuomba radhi kwake na klabu kiujumla.
“Mnasema kila mmoja anafanya makosa katika maisha hivyo jambo la kwanza linatakiwa kuwa ni je mchezaji anafikiria kuwa amefanya makosa?
“Na swali la pili ni, juhudi (za kumaliza mgogoro), zinapaswa kutoka kwangu au kwake? Hilo ni swali lingine la kujibu,” amesema Slot.