Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yajivua lawama sakata la Kariakoo Derby

Muktasari:

  • Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kanuni zinamfunga mikono kulisemea jambo la mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga ‘Kariakoo Derby’ hadharani wakati yeye si mtoa maamuzi.

Dodoma. Serikali imejiweka kando kwenye mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba ‘Kariakoo Derby’ ikisema haiwezi kuingilia mipango ya mpira kwa kuwa inakiuka sheria za ligi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi wakati akihitimisha hoja yake ya maombi ya fedha kwa mwaka 2025/26 ambapo ameomba Sh516.66 bilioni.

Awali wabunge walipokuwa wakichangia kwenye bajeti hiyo walionyesha hisia za kutaka kujua nini kilichojificha nyuma ya pazia kuanzia mazungumzo na uamuzi ambapo walimtaja Waziri kuwa alishiriki vikao vya mapatanisho lakini hajawahi kusema chochote.

Kukataliwa kwa hoja hiyo kulianzia katika mchango wa Mbunge wa Manonga Seif Gulamali alipokuwa akichangia kuhusu jambo hilo ambapo Naibu Spika Mussa Zungu alizuia akisema jambo hilo lipo mahakamani.

“Mheshimiwa Gulamali, nakuomba ujielekeza katika mambo ya kisera, kanuni ya 81 inakuzuia kusema jambo ambalo linasubiri uamuzi wake na kama utabisha nitakuingiza kwenye kanuni ya 84 halafu unajikuta huna hata sifa za kugombea,” amesema Zungu.

Aliposimama Waziri alizungumza kwa ufupi akasema “suala la ‘Derby’ siwezi kulizungumzia hapa, jambo hilo liko mahakamani na kanuni zinanifunga hapa.”

Hata hivyo kwenye upitishaji wa vifungu jambo hilo liliibuka na kuzua mvutano tena baada ya Wabunge Costantine Kanyasu (Gaita Mjini) na Joseph Msukuma (Geita Vijijini) kuliibua tena lakini Naibu Spika aliwazuia akisema hakuna mwenye mamlaka ya kuzungumzia.

Hata hivyo Msukuma alimuuliza Naibu Spika kwamba Waziri na Naibu wake walikwenda kufanya nini kwenye kikao ikiwa wanakingiwa kifua wasiulizwe wakati hawakuwa wachezaji wala viongozi wa michezo kama haitakiwi kuulizwa mbele ya kadamnasi.