Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Selemani Mwalimu, Nangu wabebeshwa mikoba Ngorongoro Heroes

Muktasari:

  • Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) 2025, zitafanyika Misri kuanzia Aprili 27 hadi Mei 18.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Wydad AC, Selemani Mwalimu ana kibarua kizito cha kuibeba timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20 ;Ngorongoro Heroes' kitakachoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo (AFCON U20) zitakazofanyika Misri baadaye mwezi huu.

Kati ya kundi la wachezaji 41 walioitwa katika kikosi cha awali cha Ngorongoro Heroes ambacho kesho Aprili 9, 2025 kitaingia kambini kujiandaa na fainali hizo, Mwalimu ndiye mshambuliaji ambaye msimu huu ameonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kufumania nyavu  kulinganisha na wengine walioitwa katika kikosi cha timu hiyo.

Ngorongoro Heroes pia imeongezewa nguvu katika safu ya ulinzi kwa ingizo la beki wa JKT Tanzania, Wilson Nangu ambaye ameonyesha kiwango bora katika Ligi Kuu msimu huu.

Mbali na Nangu, wachezaji wengine walioteuliwa kuwemo katika kikosi cha awali cha Ngorongoro Heroes baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye Ligi Kuu ni Mishamo David (Kengold), Fales Gama na pia Karim Bakari wa Coastal Union.

Nyota wengine wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi ambao wameitwa kama ilivyo kwa Mwalimu ni Emmanuel Gesabo (Muhoroni Youth, Kenya), Lucas Jayden (HJK, Finland), Paul Mhoro (Adarcon Academy, Hispania), Abdu Mandeke (Grassrunners Academy, Nigeria), Cyprian Kachwele (Vancouver FC, Canada) na Morice Sichone (Trident, Zambia).

Wachezaji 41 wanaounda kikosi hicho cha awali ni Ismail Mpank, Khatibu Mwakisiki, Gama, Anthony Remmy, Suleiman Said, Sixbert Mlingo, Nickson Mosha, Faustine Kurwa, Omary Manga, Ismaily Ally, Karim Bakari, Lameck Lawi, Vedastus Masinde, Wilson Nangu na Charles Komanya.

Wengine ni Gesabo, Muhsin Hassan, Ally Msangi, Suleiman Idrisa, Abdul Ameir, Abubakar Kiswanya, Hijja Shamte, Ahmed Pipino, Said Naushad, Goodluck Bosco, Shekhan Ibrahim, Sabry Dahari, Bakari Selemani na Zidane Sereri.

Pia kuna Jammy Simba, Jayden, Mhoro, Mandeke, Valentino Mashaka, Kachwele, Raymond Lolendi, Mwalimu, Mishamo David, Jackson Seluja na Sichone.