Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu Mudathir, Mzize kuchomolewa Stars

Muktasari:

  • Kikosi cha Taifa Stars kitaingia kambini Juni 2,2025 kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) na mashindano ya COSAFA dhidi ya Eswatini na Madagascar.

Dar es Salaam. Nyota wanne wa timu ya Taifa ya wakubwa ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars', hawatokuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachocheza mechi tatu mwezi ujao dhidi ya timu za Afrika Kusini, Eswatini na Madagascar mwezi ujao kutokana na majeraha.

Wachezaji hao ni nahodha Mbwana Samatta anayechezea PAOK ya Ugiriki, Novatus Miroshi anayeitumikia Goztepe ya Uturuki, na Mudathir Yahya na Clement Mzize wanaoichezea Yanga.

Kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman 'Morocco' amesema kuwa amewasiliana na wachezaji hao pamoja na madaktari wanaowatibu na kujiridhisha kuwa hawatoweza kuitumikia timu hiyo kwa vile kwa sasa wanauguza maumivu yao.

"Nimejaribu kuongea na wachezaji wote tegemeo kwa sababu tunataka kwenda kamili mechi na Bafana Bafana. Kapteni nimeongea naye kwa upana wake akaniambia hayuko vizuri kwa sasa yeye mwenyewe binafsi na nimejaribu kuongea na daktari wake na nimejiridhisha.

Nova (Miroshi) stori inayofanana na hiyo. Lakini tumemuacha na Mzize (Clement) ana maumivu ya misuli vilevile, Mudathir. Binafsi nimeongea nao na madaktari wao," amesema Morocco.

Kikosi kilichoitwa kina wachezaji 28 na Morocco amesema kuwa malengo ni kuwaandaa wachezaji kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) mwaka huu na pia kuanza kuwapan uzoefu vijana kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2027.

"Tuna CHAN ambayo nafikiri Agosti kwa hiyo tunajaribu kuona potential lakini tuna afcon 2027 nafikiri hizi mechi zitatusaidia kuendeleza wachezaji," amesema Morocco.

Wachezaji 28 wanaounda kikosi cha Taifa Stars ni Yakoub Suleiman, Ally Salim, Hussein Masaranga, Antony Remy, Miraji Abdallah, Shomari Kapombe, Lusajo Mwaikenda, Vedastus Masinde, Wilson Nangu, Mohamed Hussein, Ibrahim Ame, Pascal Msindo na Alphonce Mabula.

Wengine ni Ibrahim Abdulla, Dickson Job, Abdulrahim Bausi, Idrisa Stambuli, Abdulrazack Hamza, Ahmed Pipino, Yusuph Kagoma, Sheikhan Khamis, Fiesal Salum, Valentino Mashaka, Kibu Denis, Simon Msuva, Iddy Selemani, Mishamo Daudi na Selemani Mwlaimu.

Juni 6, 2025, Taifa Stars itacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Bafana Bafana na baada ya hapo itakuwa na kibarua dhidi ya Eswatini na Madagascar katika mashindano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA).