Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo akaribia rekodi ya mabao

Muktasari:

  • Kwa sasa, analenga kudumisha kiwango chake bora akiwa na Al-Nassr, baada ya kufunga mabao 12 katika michezo tisa msimu huu. Baada ya mapumziko ya hivi karibuni.

Riyadh, Saudi Arabia. Cristiano Ronaldo ameendelea kung’ara baada ya kufunga bao lake la 40 mwaka huu na kuendelea kukaribia ndoto ya kufikisha mabao 1,000 katika taaluma yake ya soka. Nyota huyo wa Ureno alifunga mabao mawili (brace), akiwa na Al-Nassr katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Al Akhdoud Jumamosi na kufikisha jumla ya mabao 956.

Mmoja wa wafuasi wake wakubwa, Piers Morgan, alitumia mitandao ya kijamii baada ya mabao hayo mawili kutangaza kuwa Ronaldo ndiye mfungaji bora zaidi wa mabao katika historia ya soka. Aliandika: “Haachi kufunga mabao. Popote duniani, kwa timu yoyote. Watu wanaweza kubishana kuhusu nani ni GOAT wa soka, lakini hakuna mjadala kuhusu nani ni mfungaji bora na asiyechoka zaidi. Ni Cristiano Ronaldo.”

Ronaldo mwenye miaka 40 mwenyewe pia aliwajulisha wafuasi wake milioni 105 kwenye X kwa ujumbe mfupi: “Kazi ngumu ndiyo njia ya mafanikio!”

Uthabiti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 ni wa kushangaza. Sasa amefunga zaidi ya mabao 40 katika miaka 14 tofauti ya kalenda ndani ya taaluma yake. Msimu wake bora zaidi ulikuwa mwaka 2013 alipofunga mabao 63 katika mashindano yote ya klabu na timu ya taifa.

Nyota huyo wa Ureno bado yuko katika hali bora ya kimwili, na hivi karibuni alishiriki picha bila shati kuonyesha mwili wake uliojengeka vizuri. Katika mahojiano na Piers Morgan mwezi uliopita, alisema anaamini bado ana mwaka mmoja au miwili kabla ya kustaafu.

Ronaldo anazingatia sana mazoezi ya Pilates, kuogelea mara kwa mara, na kwenda mazoezini mara tano kwa wiki. Ratiba yake inajumuisha dakika 25–30 za mazoezi ya moyo (cardio), mbio za kasi ya juu na mazoezi maalum ya kuongeza nguvu za misuli. Kwa jumla, hufanya mazoezi kwa saa tatu hadi nne kila siku.

Kuhusu lishe, badala ya kula milo mitatu ya kawaida (kifungua kinywa, chakula cha mchana na chakula cha jioni), Ronaldo hupendelea kula milo midogo sita kwa siku: kifungua kinywa, brunch, chakula cha mchana, vitafunwa, supper na chakula cha jioni.

Kujituma kwake bila kuchoka ili kupata kila tone la ubora katika taaluma yake kunafanya kufikisha mabao 1,000 kuonekana kuwa jambo lisiloepukika. Pia anailenga taji la Kombe la Dunia nchini Marekani mwaka ujao, ambalo lingeweza kuwa hitimisho la hadithi ya kusisimua katika taaluma yake.

Kwa sasa, analenga kudumisha kiwango chake bora akiwa na Al-Nassr, baada ya kufunga mabao 12 katika michezo tisa msimu huu. Baada ya mapumziko ya hivi karibuni, amerejea kwa kasi, na ushindi huo umeifanya Al-Nassr kushinda michezo yote 10 msimu huu hadi sasa, wakiongoza Ligi Kuu ya Saudi Arabia kwa tofauti ya pointi nne.