Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo azua gumzo akikutana na Trump leo

Muktasari:

  • Ureno ni miongoni mwa timu ambazo zimefuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 nchini Marekani, Canada na Mexico ambapo Ronaldo anategemewa kuwa miongoni mwa nyota watakaokuwa kikosini.

Cristiano Ronaldo leo atakutana na Rais wa Marekani, Donald Trump ikiwa ni mara ya kwanza kwa nyota huyo wa Ureno kutua ndani ya ardhi ya nchi hiyo baada ya kipindi cha takribani muongo mmoja.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 40 anayeichezea Al Nassr hajawahi kupigwa picha ndani ya ardhi ya Marekani tangu alipopata tuhuma za kumbaka Mwalimu Kathryn Mayorga mwaka 2017.

Akitoa maelezo ya madai ya unyanyasaji wa kijinsia katika mahojiano ya 2017 na gazeti la Ujerumani, Der Spiegel, Mayorga alidai Ronaldo alimbaka katika hoteli ya Las Vegas mwaka 2009.

Mwanamke huyo aliripotiwa kufikia suluhu nje ya mahakama na Ronaldo mwaka 2010, lakini aliibua shutuma zake miaka saba baadaye katika jitihada za kutafuta zaidi ya Dola 375,000 (Sh911 milioni) alizopokea.

Kesi dhidi ya Ronaldo, ambaye mara kwa mara na kwa ukali alikanusha tuhuma hizo, ilitupiliwa mbali na jaji wa Marekani mwaka 2022 kwa sababu wakili wa mshtaki huyo alitegemea rekodi zilizovuja na kuibiwa.

Ronaldo, ambaye ziara yake ya mwisho nchini Marekani ilikuwa 2016 aliposherehekea ushindi wa Ureno wa Ubingwa wa Ulaya huko Las Vegas, sasa anatarajiwa kukaribishwa na Trump katika Ikulu ya White House leo kama sehemu ya ziara ya serikali ya Saudi Arabia.

Safari adimu ya Ronaldo kuvuka Atlantiki inakuja miezi saba kabla ya michuano ya Kombe la Dunia 2026, ambayo itaandaliwa Marekani, Canada na Mexico.

Ureno pia wako tayari kumenyana na Timu ya Taifa ya Marekani kwenye Uwanja wa Mercedes-Benz huko Atlanta mnamo Machi 2026, huku Ronaldo akitarajiwa kushiriki katika mechi ya kirafiki kabla ya Kombe la Dunia.

Mashabiki walifuatilia kwa hamu ndege ya Ronaldo kutoka Riyadh kuelekea Washington DC Jumatatu usiku, wakibaini kwamba nyota huyo wa Ureno na mchumba wake Georgina walitarajiwa kutua leo saa 10:36 jioni

Georgina, 31, aliingia kwenye mitandao ya kijamii kusambaza picha za ndege hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.