Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ramovic apata mchoro wa robo fainali CAF

Muktasari:

  • Yanga yenye pointi saba ikiwa kwenye nafasi ya tatu ya kundi hilo itahitaji ushindi ili ifuzu huku MC Alger yenye pointi nane ikihitaji sare au ushindi kujihakikishia nafasi ya pili inayowaniwa na timu zote mbili.

Yanga imerejea nchini leo alfajiri ikitokea Mauritania iliposhinda mechi ya pili kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku kocha mkuu wa timu hiyo Saed Ramovic akieleza mpango alionao ili kuichapa MC Alger kwenye mchezo wa mwisho wa kundi A.

Yanga itakutana na MC Alger Jumamosi Januari 18, kwenye mchezo wa mwisho wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao kati ya timu hizo mbili moja itatakiwa kuungana na Al Hilal ya Sudan kwenda Robo Fainali.

Yanga yenye pointi saba ikiwa kwenye nafasi ya tatu ya kundi hilo itahitaji ushindi ili ifuzu huku MC Alger yenye pointi nane ikihitaji sare au ushindi kujihakikishia nafasi ya pili inayowaniwa na timu zote mbili.

Akizungumza na Mwananchi, Ramovic amesema amewazuia wachezaji wake kushangilia ushindi dhidi ya Al Hilal akisema anataka kumuona kila mmoja akiweka mawazo yake kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Algier kwa kuwa ndiyo umeshikilia hatma yao ya kufuzu kwenda robo fainali.

Kocha huyo alisema amefurahishwa na namna wachezaji wake walivyojituma kwenye mechi  tatu za mwisho akiona morali yao inaendelea kupanda na sasa wana mlima kwenye mechi ya mwisho ambayo kwao ni kama fainali.

Kocha huyo Mjerumani ambaye anaendelea kuibadilisha timu hiyo kwa kasi alisema anajua mchezo huo utakuwa mgumu lakini ana imani na namna wachezaji wachezaji wake wanaonyesha njaa ya kutafuta ushindi.

"Hii mechi (dhidi ya Al Hilal) imekwisha niliwaambia wachezaji baada ya kutoka ndani ya uwanja kila mmoja asitishe furaha yake, tunatakiwa kujiona kama hatujafanya kitu na tukitakiwa kwenda kufanya kitu kikubwa kwenye mchezo ujao wa nyumbani.

"Tunatakiwa kushinda mechi ya mwisho kwa nguvu, haitakuwa rahisi MC Alger nao wanaopitia mabadiliko kwenye timu yao tofauti na walivyoanza mechi za makundi, tunachotakiwa ni kuongeza umakini kwenye mechi hii ya mwisho.

"Tutakuwa nyumbani na wao walishinda dhidi yetu wakiwa kwao, tumekuwa na mabadiliko mazuri ndani ya timu yetu tofauti na mechi mbili za kwanza tulizocheza na tumeanza kuimarika kwa nguvu, nawapongeza sana wachezaji wangu lakini wanatakiwa kutambua tunakwenda kucheza fainali ngumu itakayobeba heshima yetu.

Hata hivyo, Ramovic amekiri kwamba timu yake ilistahili kushinda kwa mabao mengi dhidi ya Al Hilal kwa kuwa walitengeneza nafasi nyingi lakini wakashindwa kuzitumia, jambo ambalo inabidi alifanyie kazi ili lisijirudie kwenye mchezo ujao.

"Ni kweli tungeweza kupata mabao zaidi tulitengeneza nafasi nyingi lakini ile ni mechi ambayo tukitakiwa kushinda tena dhidi ya timu iliyocheza kwa ubora mechi zake nne za kwanza, ilikuwa mechi ngumu na yenye presha kubwa.

"Tutazungumza na wachezaji kuwaongezea utulivu ili makosa ya kupoteza nafasi yasiendelee, tukicheza kwa umakini zaidi ya ule tuliouonyesha dhidi ya TP Mazembe tunaweza kufanikiwa."