Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pogba rasmi kurejea uwanjani msimu ujao

Muktasari:

  • Pogba ameonekana mara kadhaa akifanya mazoezi na vijana wa Manchester United huko Florida, Marekani, ikiwa ni sehemu ya harakati za kujiweka fiti kabla ya msimu mpya kuanza.

Nyota wa zamani wa Manchester United na Juventus, Paul Pogba, amerejea rasmi kwenye soka la ushindani baada ya kuripotiwa kukubaliana na mkataba wa miaka miwili na klabu ya Monaco inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti la Le Parisien la Ufaransa, Pogba amekubali kupunguza thamani yake ili kufanikisha kurejea kwake, akitia saini kandarasi hiyo licha ya kupunguziwa mshahara mkubwa aliozoea. Inadaiwa kuwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili yalidumu kwa siku kadhaa kabla ya kufikia makubaliano rasmi Jumapili iliyopita.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alifungiwa kucheza soka kwa miaka minne baada ya kupatikana na kosa la kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, lakini adhabu hiyo ilipunguzwa hadi miezi 18 baada ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kuthibitisha kuwa alitumia kwa bahati mbaya dawa ya DHEA kiambato kinachochochea uzalishaji wa testosterone. Hata hivyo, mahakama hiyo ilieleza kuwa kiambato hicho huathiri zaidi wanawake, si wanaume.

Pogba, ambaye hajacheza mechi yoyote tangu Septemba 2023, ameripotiwa kuanza maandalizi ya maisha mapya Monaco, ikiwemo kupangisha makazi mapya. Alitembelea mji wa kifalme wa Monaco mapema Juni kukutana na viongozi wa klabu hiyo na kutathmini mazingira kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho.

Kwa sasa, Pogba ameonekana mara kadhaa akifanya mazoezi na vijana wa Manchester United huko Florida, Marekani, ikiwa ni sehemu ya harakati za kujiweka fiti kabla ya msimu mpya kuanza. Alipigwa picha akiwa na Leny Yoro (aliyesajiliwa kutoka Lille msimu uliopita) na Kobbie Mainoo wa Manchester United, huku akiwa amevalia jezi ya zamani ya Juventus, akionyesha dhamira ya kurudi katika kiwango chake cha juu.

Endapo dili lake na Monaco litakamilika, Pogba atakuwa anacheza kwa mara ya kwanza kabisa katika Ligi Kuu ya Ufaransa licha ya kuiwakilisha timu ya taifa ya Ufaransa mara 91 na kushinda Kombe la Dunia mwaka 2018, hajawahi kucheza ligi ya nyumbani tangu aanze kucheza soka. Monaco ilimaliza msimu uliopita katika nafasi ya tatu, ikizidiwa na Marseille na mabingwa Paris Saint-Germain, hatua inayowapa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu wa 2025/2026.