Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nini kinaitafuna Simba?

Muktasari:

  • Chanzo hicho ambacho kipo ndani ya bodi kinasema kama vipengele hivyo vitapita basi upande wa mwekezaji utakuwa hauna nguvu tena klabuni hapo na kila kitu kitaendeshwa na upande wa wanachama.

Kuna nini Simba? Hili ndiyo swali ambalo mashabiki wa timu hiyo wanajiuliza zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya mkutano mkuu wa klabu hiyo, huku kukiwa na makundi mawili ambayo yanaonekana kupishana kwenye baadhi ya mambo.

Simba inafanya mkutano wake mkuu wa kikatiba Jumapili ijayo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, ambapo wanachama wa klabu hiyo watajadili kuhusu mustakabali wa timu hiyo kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Hata hivyo, kumekuwa na vita kubwa mtandaoni kutoka kwenye makundi mawili tofauti ya timu hiyo, kundi moja likionekana kuwa upande wa mwekezaji wa timu hiyo, Mohammed Dewji na lingine likiwa upande wa wanachama ambao unaongozwa na Murtaza Mangungu.

Inadaiwa kuwa vita kubwa ya makundi hayo ni baadhi ya ajenda ambazo zitakwenda kujadiliwa kwenye mkutano huo, yakiwemo mabadiliko makubwa ya katiba ambayo yanaweza kuliondoa kundi moja kwenye usimamizi wa jumla wa klabu hiyo.

Ajenda ya mabadiliko ya katiba ndiyo ambayo inaonekana kuwa na vita kubwa kwa kuwa kama ikipita inaonyesha kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa ya kiundeshaji kwenye klabu hiyo hali ambayo inadaiwa imesababisha mmoja wa mabosi wa timu hiyo kuongezewa mkataba mpya kimya kimya kabla ya mkutano huo ili kuliunga mkono kundi mojawapo.

"Mtendaji kapewa mkataba ni kweli bodi hatufahamu, lakini inaonekana ni ili aweze kuliunga mkono kundi mojawapo ambalo lina jambo lake kwenye mkutano mkuu ujao, sidhani kama ni sawa kwa sasa kuwa na makundi, Simba inahitaji watu wenye umoja kwa kuwa kuna mambo mengi ya kufanya, lakini subiri tuone itakavyokuwa kwenye mkutano lakini mambo hayatakuwa rahisi," mmoja wa wajumbe wa Bodi alilieleza Mwananchi.

Akizungumza na kituo cha Redio cha Crown FM, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori amesema kuwa kuna watu wapo nje ya Simba ambao hawaitakii mema klabu hiyo na wanataka kufanya fujo kwenye mkutano mkuu ujao.

"Kuna kundi lipo nje ya Simba ndiyo linaleta hizi chokochoko, watu walishaongoza muda wao umemalizika wananchotakiwa ni kuiunga mkono timu siyo kufurahia timu ikiwa haijafanyi vizuri.

"Huwezi kuamini kuwa watu wanafuarahi Simba ikipoteza mchezo na juzi wamecheka sana tulipofungwa na walishakuwa viongozi wa timu huko nyuma, hii siyo sawa hata kidogo, wakati mimi nilipomaliza uongozi wangu nilikuwa hadi nagombana na watu kuhakikisha Simba inafanya vizuri," alisema Magori.


Nini kinakwenda kujadiliwa:

Pamoja na mambo mengine mengi ambayo yanatarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano mkuu wa Simba, chanzo cha ndani kimelieleza Mwananchi kuwa fukuto kubwa lipo kwenye vipengele vya katiba ambavyo vinatakiwa kupitishwa na mkutano huo mkuu ambavyo vinaweza kubadilisha mwenendo mzima wa klabu hiyo.

Chanzo hicho ambacho kipo ndani ya bodi kinasema kama vipengele hivyo vitapita basi upande wa mwekezaji utakuwa hauna nguvu tena klabuni hapo na kila kitu kitaendeshwa na upande wa wanachama.

"Unajua kwa utaratibu wanachama wana asilimia 51 na hawa kisheria ndiyo wanatakiwa kutoa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi lakini hapo nyuma kwa kipindi chote mwenyekiti alikuwa anatoka upande wa mwekezaji ambao wana asilimia 49, sasa kuna kipengele kwenye katiba ambacho kinatakiwa kupitishwa kuwa upande wa wanachama ndiyo unatakiwa kutoa kiongozi wa bodi, hivyo timu iwe inaendeshwa upande wa wanachama," kilisema chanzo hicho cha uhakika.

Hata hivyo, alisema jambo lingine ambalo linaonekana kuwa litakuwa na mvutano mkubwa kwenye mkutano huo ni kuwepo kipengele kwenye katiba ambacho kinataka timu hiyo iwe na wawekezaji na siyo mwekezaji kama hali ilivyo sasa.

"Katiba pia inataka kuwe na wawekezaji na siyo mwekezaji kama ilivyo sasa, hii ina maana kuwa hisa asilimia 49 ambazo kwa sasa zinaonekana kuwa zinamilikiwa na mtu mmoja, zigawanywe kwa watu wengi, kama kuna ambaye atakuwa na hisa tano, mwingine kumi na mwingine 20 sawa lakini asiwe mtu mmoja, hili nalo linaonekana kuwa linawagawa wajumbe na wanachama kwa kuwa wengine wanaamini mwekezaji wa sasa anafanya kazi yake vizuri, lakini wengine wanaamini wakiwa wengi watafanya vizuri zaidi hapa ndiyo shida nyingine ilipo."

Inaelezwa kuwa kipengele cha tatu ambacho kipo kwenye katiba hiyo ni kuwa na Kamati ya Utendaji badala ya Bodi ya Wakurugenzi kwa kuwa mchakato wa uwekezaji bado haujapita, jambo lingine ambalo linawagawa wananchama hai wa timu hiyo.


Hasanoo apiligilia msumari

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Simba Hassan Hasanoo alisema kuwa anaamini kisheria upande wa wanachama ndiyo wanatakiwa kuendesha klabu hiyo kwa mujibu wa sheria.

"Kuna upotoshaji mkubwa unafanyika, lakini hiki kitu kinachoitwa uwekezaji serikali ilishakifuta muda mrefu sana, hakuna bodi ya pande mbele Simba mimi naunga mkono asilimia mia moja wanachama kuendesha klabu."

Kama itakuwa hivyo ina maana kuwa wajumbe ambao wataongoza klabu hiyo watatoka upande wa wanachama pekee na hatakutakuwa na wajumbe nane wa upande wa mwekezaji, hivyo Magori na wanzake ambao waliteuliwa na Mo Dewji hawatakuwa na mamlaka yakuwemo klabuni hapo kama viongozi.