Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngorongoro Heroes yaangukia kundi la mtego AFCON U20

Muktasari:

  • Timu nne zinazotinga nusu fainali katika Fainali za AFCON U20 zinajihakikishia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa vijana wa umri huo.

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ imepangwa kundi A katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo (AFCON U20) 2025 zitakazofanyika Misri baadaye mwezi huu.

Kundi hilo A linaundwa na timu tano ambazo ni Misri, Zambia, Ngorongoro Heroes, Sierra Leone na Afrika Kusini.

Ni kundi lenye mchanganyiko wa timu zenye uzoefu na mafanikio kwenye mashindano hayo na nyingine  zinashiriki kwa mara ya kwanza.

Mwenyeji Misri ndio timu tishio zaidi katika kundi hilo kwa vile inashika nafasi ya pilk kwa kutwaa taji hilo mara nyingi ikifanya hivyo mara nne ambazo ni 1981, 1991, 2003 na 2013.

Misri imeshika nafasi ya pili mara moja na imewahi kumaliza katika nafasi ya tatu mara tatu.

Zambia ni timu nyingine iliyowahi kuonja mafanikio kwenye kundi A ambapo imetwaa ubingwa mara moja ambayo ni mwaka 2017 na imeshika nafasi ya nne mara tatu ambazo ni 1991, 1999 na 2007.

Hii ni mara ya kwanza kwa Afrika Kusini kushiriki fainali hizo huku Ngorongoro Heroes ikishiriki kwa mara ya pili.

Ngorongoro Heroes ilishiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza katika fainali za 2021 ambapo iliishia katika hatua ya makundi pindi zilipofanyika Mauritania.

Mabingwa wa kihistoria wa fainali hizo Nigeria ambao wametwaa taji hilo mara saba, wamepangwa katika kundi B na timu za Tunisia, Kenya na Morocco.

Bingwa mtetezi, Senegal amepangwa katika kundi C na timu za Jamhuri ya Afrika ya Kati, DR Congo na Ghana.

Fainali za AFCON U20 zimepangwa kufanyika Misri kuanzia Aprili 27 hadi Mei 18.