Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapinzani Ngorongoro Heroes hadharani leo

Muktasari:

  • Ngorongoro Heroes inashiriki AFCON U20 2025 baada ya kuchukua ubingwa wa mashindano ya kuwania kufuzu kupitia kanda ya baraza la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ leo itafahamu kundi itakalopangwa na wapinzani itakaocheza nao kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri kama huo (AFCON) mwaka huu huko Misri.

Fainali hizo zitafanyika kuanzia Aprili 27 hadi Mei 18 zikishirikisha timu 13 za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 20.

Katika droo ya leo itakayofanyika katika makao makuu ya Chama cha Mpira wa Miguu Misri (EFA) kuanzia saa 12 jioni kwa muda wa Afrika Mashariki, makundi matatu yatapangwa.

Kundi A litakuwa na timu tano na kundi B na C kila moja litakuwa na timu nne ambapo wenyeji Misri watakuwa kundi A,  Nigeria itakuwa kundi B na bingwa mtetezi Senegal itakuwa kundi C.

Katika upangaji wa makundi hayo, Tunisia, Zambia na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo zilifuzu fainali zilizopita, zitawekwa katika chungu cha kwanza na Morocco, Ngorongoro Heroes, Sierra Leone, Kenya, Afrika Kusini, Ghana  na  DR Congo zitakuwa katika chungu cha pili.

Hii ni mara ya pili kwa Ngorongoro Heroes kushiriki fainali za AFCON U20 ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni 2021 pindi yalipofanyika Mauriatania ambapo timu hiyo iliishia katika hatua ya makundi.

Timu nne zitakazoingia nusu fainali kwenye fainali za AFCON U20 2025 zitafuzu Fainali za Kombe la Dunia kwa vijana wa umri huo zitakazofanyika Chile baadaye mwaka huu.