Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MZEEWA FACT: Europa League 2025 ni fainali ya liwalo na liwe

Muktasari:

  • Ukiwaangalia wana fainali wa msimu huu, Liwalo la Liwe, utaona kabisa kwamba Wenger yuko sahihi kuikataa kanuni hii.

Liwalo na Liwe ni msemo uliojipatia umaarufu mkubwa sana mitandaoni kuanzia mwaka 2019, baada ya mkuu wa mkoa wa Tabora wa wakati huo, Mh. Aggrey Mwanri, kuutumia alipokuwa akiongea na bodaboda mjini Tabora.

'Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ni lazima ituoneshe ni mahali gani (bodaboda) watapaki. Na kama haisemi basi ni vurugu, mimi nitasema tu, "Jamani eh, Liwalo na Liwe" 

Namna alivyojikunja kunja na kucheza na sauti lake zito wakati akiyatamka maneno ya LIWALO NA LIWE, ndio ikasababisha msemo huo kuteka mitandao ya kijamii.

Nyimbo nyingi zikatungwa kwa kutumia jina hilo, kama Harmonize, Lavalava, Lady Jaydee akishirikiana na Rama Dee na hata Mbosso katika wimbo wake wa Huyu Hapa, hakutaka msemo huo umpite bila kuutumia.

Lakini msemo huo ulienda mbali kiasi cha kuhama kutoka maana yake ya asili na kugeuka kuwa kama kiwakilishi cha nafsi.

Yaani inapotokea watu wawili wenye kufanana kwa matendo yao ya yasini na faida, basi mmoja atakuwa Liwalo na mwingine Liwe.

Ikaja hadi kwenye michezo, pale timu mbili zenye mfululizo wa matokeo mabaya zinapokutana na zenyewe zikawa Liwalo na Liwe.

Na hiki ndicho kinachoenda kutokea kwenye fainali ya Europa League pale Manchester United na Tottenham Hotspur watakapokutana Mei 21 mwaka huu kwenye dimba la San Mames mjini Bilbao nchini Hispania.

Timu hizi mbili zinakutana huku zote zikiwa katika hali mbaya sana kwenye ligi ya nyumbani, zikishindana kufungwa kila uchao.

Ni ajabu sana kwamba ni kama zilijichagua zenyewe zikutane kwani stori yao ni kama ile ya LIWALO NA LIWE.

i. Zinatumia wimbo mmoja

Manchester United na Tottenham Hotspur ni timu zinazotumia wimbo mmoja kama wimbo rasmi wa klabu.

Wimbo huo ni Glory Glory, ambapo kila mmoka kaweka jina lake ili kuwe tofauti.

Glory Glory Man. United x3

-As the reds go marching on, on, on

Glory glory Tottenham Hotspur x3

-And the Spurs go marching on

Asili ya wimbo huu ni wimbo wa "Battle Hymn of the Republic" yaani wimbo wa mapambano wa Jamhuri, uliotungwa na mwanaharakati wa Marekani, Julia Ward Howe, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Tottenham Hotspur ndiyo walikuwa wa kwanza kuufanya wimbo huu kama wimbo wao rasmi, msimu wa 1960/61, waliposhinda ubingwa wa Ligi.

Huo ndiyo ubingwa wao wa mwisho wa ligi, kwani baada ya hapo hawajashinda tena hadi sasa.

Manchester United wakawafuata baadaye mnamo mwaka ya 1983 nao wakaanza kuutumia wimbo huu kama wimbo wao rasmi. 

ii. Vibonde kwenye Ligi

Zikiwa katika nusu ya pili ya msimamo wa ligi; Manchester United ya 16 na Tottenham Hotspur ya 17, timu hızı mbili zipo katika msimu mbaya zaidi katika historia yao ya zama za ligi kuu.

Tottenham wanaelekea kuvunja rekodi yao ya msimu 1993/94, walipomaliza kwenye nafasi ya 15.

Na Manchester United wanaelekea kuvunja rekodi yao ya msimu wa 2023/24, walipomaliza katika nafasi ya 8.

Hadi sasa Tottenham Hotspur imepoteza mechi 21, huku Manchester United ikipoteza mechi 18.

New Content Item (1)

Ndio maana Wenger hataki

Wakati akiitumikia Arsenal kama kocha, Arsene Wenger alikuwa akifanya maajabu ambayo hakuna aliyeyatarajia.

Angeweza kwenda klabu fulani ndogo au kwenye akademi ya timu fulani na kuchukua kachezaji fulani ambako hakuna aliyekadhania.

Halafu anakatengeneza na kukageuza kuwa moto wa kuotea mbali ndivyo alivyofanya kwa wachezaji kama Kolo Toure.

Alimtoa Asec Mimosas ya Ivory Coast, hadi Arsenal moja kwa moja na kugeuka kuwa mhimili wa timu hiyo kiasi cha kuisaidia kumaliza ligi pasipo kupoteza mchezo 2003/24 na kuifikisha fainali ya ligi ya mabingwa 2005/06.

Kutokana na mambo kama hayo, mashabiki wa Arsenal wakawa hawana shaka naye hata kidogo kiasi cha kuja na msemo wa WENGER KNOWS BEST...yaani Wenger anajua zaidi.

Hata akifanya jambo la hovyo, wao watamuunga mkono wakiamini Wenger hakosei kwa sababu anajua zaidi.

Miaka mingi imepita tangu Arsene Wenger atengane na Arsenał, lakini bado msemo ule wa mashabiki unaakisi maono ya Wenger.

Hiki karibuni alirudi tena kwenye vichwa vya habari baada ya kukosoa kanuni ya UEFA ya kuruhusu bingwa wa Europa League kupata tiketi ya kushiriki ligi ya mabingwa msimu unaofuata.

Wenger alisema hiyo sio sawa, akitaka bingwa wa Europa League apate tiketi ya moja kwa moja ya kutetea ubingwa wake bila kuhamia mashindano mengine.

Ukiwaangalia wana fainali wa msimu huu, Liwalo la Liwe, utaona kabisa kwamba Wenger yuko sahihi kuikataa kanuni hii.

Timu moja kati ya Tottenham Hotspur na Manchester United ambazo zinaweza kumaliza ligi juu ya mstari wa kushuka daraja, itafuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao aibu gani hii?