Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mukombozi afutiwa kadi ya Simba, refa akaushiwa

Muktasari:

  • Wakati kamati hiyo ikiifuta kadi hiyo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa Smarti aliyetoa maamuzi hayo ya kadi kwa Mulokozi.

Dar es Salaam. Beki wa Namungo, Derrick Mukombozi hatimaye amefutiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyopewa kwenye mchezo dhidi ya Simba.

Mukombozi alipewa kadi hiyo iliyozua utata na mwamuzi Japhet Smarti kutoka Katavi, kwenye mchezi dhidi ya Simba baada ya beki huyo kuwa kwenye harakati za kumzuia mshambuliaji Lionel Ateba.

Hata hivyo, kadi hiyo ilionekana kuwashtua wengi kutokana na mikanda ya video kuonyesha hakukuwa na tukio lolote linaloweza kusababisha adhabu ya namna hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Usimamizi wa Ligi imetangaza rasmi kwamba kadi hiyo imeondolewa kwa kile ilichosema maelezo yaliyopo kwenye ripoti ya mwamuzi hayakuwa na ushahidi wa kutosha unaoendana na marejeo ya picha mjongeo.

Wakati kamati hiyo ikiifuta kadi hiyo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa Smarti aliyetoa maamuzi hayo ya kadi kwa Mulokozi.

Kwa upande mwingine beki wa Namungo, Daniel Amoah ametozwa faini ya sh 500,000 kwa kosa la kuonekana akimwaga vimiminika kwenye goli jambo linalohusishwa na vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina tukio ambalo lilitokea kwenye mchezo huo dhidi ya Simba ambao wekundu hao walishinda kwa mabao 3-0.