Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mlinzi wa Cristiano Ronaldo alipwa Sh4.5 bilioni

Muktasari:

  • Cristiano Ronaldo analipwa mshahara wa Dola 200 milioni (Sh531 bilioni) kwa mwaka na Al Nassr inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Mlinzi wa zamani wa mshambuliaji Cristiano Ronaldo, Hichman Bukhari amefichua kuwa nyota huyo wa Al Nassr na timu ya taifa ya Ureno alikuwa akimlipa kiasi cha Pauni 850 kwa siku kama malipo ya kazi ya kumlinda.

Bukhari amesema kuwa ameifanya kazi hiyo kwa muda wa miaka minne jambo ambalo limemfanya avune kiasi cha Pauni 1.3 milioni (Sh4.5 bilioni) kwa kazi ya kumlinda staa huyo.

Mlinzi huyo amesema kwamba kazi ya kumlinda Ronaldo haikuwa ngumu kwa vile mchezaji huyo hakuwa katika hatari ya kuuliwa au kushambuliwa.

“Kazi yetu inategemea na wasifu wa mteja. Kwa suala la Cristiano ambaye nilifanya naye kazi kwa miaka minne, wasifu wake haukumweka katika hatari kubwa kwa sababu watu hawakutaka kumuua na hakuwahi kupokea vitisho vya kuuawa.

“Alikuwa anatishwa na mashabiki au wwtu ambao walitaka kumhadaa. Tunatakiwa kujua siku zote wapi tunaelekea, nani watakuwepo hapo na kusafisha sehemu za kuingilia na kutokea na pia za makutano,” alisema mlinzi huyo.

Hichman ameongeza kuwa pamoja na Ronaldo kutokuwa hatarini, alihakikisha anachukua tahadhari zote.

“Tunatakiwa siku zote kuwa na tahadhari kwamba maisha yetu yanaweza kuwa hatarini. Tunatakiwa kuwa tayari kumlinda mtu na wakati mwingine tunatakiwa kuyatoa maisha yetu kuwalinda.

“Kama natakiwa kutumia silaha, natumia. Jambo la muhimu zaidi ni kuwa na uwezo wa kufikiria kwa haraka, kutatua matatizo na kuwa na utulivu wakati wa nyakati ngumu,” amesema Hichman.

Mlinzi huyo amemtaja Ronaldo kama mtu bora ambaye amewahi kufanya naye kazi.

“Ni bosi bora zaidi kuwahi kuwa naye. Tulikuwa na uhusiano mzuri. Kufanya kazi na yeye haikuwa sawa na kufanya kazi na mtu aliye katika hatari ya kuuliwa au kutekwa.

“Tulikuwa na nyakati zisizo nzuri na waandishi wa habari na mashabiki vichaa lakini hakukuwa na kubwa,” amefichua Hichman.

Hichman ni mlinzi mwenye utaalam maalum wa kulinda watu binafsi akiwa na wafuasi zaidi ya 120,000 katika mtandao wa Instagram