Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miujiza tu kuiokoa Kagera Sugar Ligi Kuu

Muktasari:

  • Kagera Sugar inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imekusanya pointi 22.
no

Baada ya kupoteza mechi ya nyumbani kwa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa FC jana, ni miujiza tu inayoweza kuifanya Kagera Sugar ibakie katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Bao pekee la Jafari Kibaya katika dakika ya 19, limeifanya Kagera Sugar sasa kuombea Pamba Jiji kupoteza mechi zake tatu zilizosalia na yenyewe ipate ushindi katika mechi zake mbili zilizosalia ili angalau ipate fursa ya kupigania kubaki Ligi Kuu kupitia mechi za mchujo (play offs).

Bao hilo la Kibaya lilitokana na mkwaju wa penalti ambayo ilisababishwa na beki wa Kagera Sugar, Musa Mohamed kunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Lakini kama Pamba itapata pointi mbili tu katika mechi tatu ilizobakiza, Kagera Sugar itashuka rasmi daraja.

Mechi mbili ambazo Kagera Sugar imebakiza ni dhidi ya Namungo FC na Simba ambazo zote itacheza ugenini.

Pamba Jiji imebakiza mechi tatu ambazo mojawapo ni leo ugenini dhidi ya Kengold na nyingine mbili nyumbani dhidi ya JKT Tanzania na KMC.

Kocha wa Kagera Sugar, Juma Kaseja amesema kuwa bado wana tumaini la kubaki kwenye Ligi Kuu.

“Mimi ni mshindani tutaendelea kupambana katika hizo mechi mbili zilizobakia kuona tutapata nini na msimamo wa ligi ukoje,” amesema Kaseja.

Tayari timu moja imeshashuka daraja ambayo ni Kengold inayoshika mkia kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 16.