Mexico yaanza vyema, kadi nyekundu zikimwagika
Baadhi ya wachezaji wa Mexico wakishangilia moja ya bao katika ushindi wa 2-0 waliopata kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Afrika Kusini. Picha na Mtandao
Muktasari:
- Afrika Kusini imebakiza mechi mbili kwenye kundi A dhidi ya Korea Kusini na Jamhuri ya Czech.
Mexico imeanza vizuri Fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo dhidi ya Afrika Kusini.
Katika mchezo huo, mabao ya Mexico yamefungwa na Julian Quinones na Raul Jimenez.
Ni mchezo ambao umeweka historia isiyovutia ya idadi kubwa ya kadi nyekundu ambapo zimetoka tatu.
Afrika Kusini wameonyeshwa kadi nyakundu mbili na wenyeji Mexico wameonyeshwa kadi nyekundu moja.
Kadi nyekundu za Afrika Kusini ni zile walizoonyeshwa wachezaji Yaya Sithole na Themba Zwane na kwa upande wa Mexico alionyeshwa Cesar Montes.
Kwa kuonyeshwa kadi nyekundu hizo, Zwane na Sithole watakosa mechi mbili zilizobakia za Afrika Kusini kwemye kundi A.
Mechi hizo ni dhidi ya Korea Kusini na Jamhuri ya Czech.
Mchezo huo umechezeshwa na refa Wilton Sampaio kutoma Brazil.