Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Deni la Serikali lafikia Sh114.34 trilioni

Muktasari:

  • Deni la Serikali limeongezeka hadi kufikia Sh114.34 trilioni Machi mwaka huu kutoka Sh104.93 trilioni kipindi kama hicho mwaka 2025 sawa na ongezeko la asilimia 8.97. Kati ya kiasi hicho, deni la ndani lilikuwa Sh38.44 trilioni na deni la nje lilikuwa Sh75.89 trilioni.

Dar es Salaam. Deni la Serikali limeongezeka hadi kufikia Sh114.34 trilioni Machi mwaka huu kutoka Sh104.93 trilioni kipindi kama hicho mwaka 2025 sawa na ongezeko la asilimia 8.97.

Kati ya kiasi hicho, deni la ndani lilikuwa Sh38.44 trilioni na deni la nje lilikuwa Sh75.89 trilioni.

Hayo yamesemwa wakati wa uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/27 bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi Juni 11, 2026 uliofanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo.

“Ongezeko la deni linatokana na Serikali kuendelea kupokea mikopo mipya na ya zamani kutoka vyanzo vya ndani na nje kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo,” amesema Profesa Kitila.

Licha ya deni hilo kuongezeka, bado ni himilivu huku tathmini iliyofanyika Novemba 2025 ilibainisha kuwa deni la Serikali ni himilivu katika kipindi cha muda wa kati na mrefu na viashiria vya deni vilionesha kuwa mwaka 2025/26

Tathmini hiyo hufanyika kwa kuzingatia vigezo vya uhimilivu, ikiwemo uwiano wa deni halisi kwa Pato la Taifa, uwiano wa deni halisi kwa malipo ya nje na uwiano wa malipo ya deni kwa mapato ya ndani na mapato yatokanayo na mauzo ya nje.

Kwa mujibu wa tathmini hiyo, deni la Serikali ni himilivu katika kipindi cha muda wa kati na mrefu na viashiria vya deni vilionesha kuwa mwaka 2025/26, thamani ya sasa ya deni la nje kwa Pato la Taifa ni asilimia 24.4 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 40.

“Pia thamani ya sasa ya deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 123.1 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 180, ulipaji wa deni la nje kwa kutumia mapato yatokanayo na mauzo ya nje ni asilimia 12.8 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 15 na ulipaji wa deni la nje kwa kutumia mapato ya ndani ni asilimia 15.4 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 18,” amesema Profesa Kitila.

Kwa upande wa viashiria vya deni la nje na ndani, thamani ya sasa ya deni kwa Pato la Taifa ni asilimia 39.6 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55.

Kuhusu uwezo wa nchi kukopa na kulipa madeni katika masoko ya Kimataifa Februari 2026, kampuni ya Moody’s Investors Services ilifanya mapitio ya uchumi wa Tanzania ili kubaini uwezo wa nchi kukopesheka.

Katika mapitio hayo, Tanzania iliendelea kubaki katika daraja la B1 ikiwa ni mtazamo thabiti kama ilivyokuwa Machi 2025. Kwa upande mwingine, Kampuni ya Fitch Ratings ilifanya mapitio kama hayo Machi 2026 na kuipa Tanzania alama ya B+ ikiwa na mtazamo thabiti (Stable Outlook) kama ilivyokuwa mwaka 2025.

“Hii inatokana na kuendelea kuwepo kwa misingi imara ya uchumi, ikiwemo ukuaji Pato la Taifa, uthabiti wa mfumuko wa bei, na deni la Serikali himilivu,” amesema.

Amesema matokeo haya yanaimarisha imani ya wawekezaji wa ndani na nje kuhusu uthabiti wa uchumi na uwezo wa Serikali kusimamia deni na hivyo kuwezesha kupunguza gharama za kukopa katika masoko ya kimataifa na kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.