Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi za uamuzi Ligi ya Mabingwa Afrika

Muktasari:

  • Bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika anapata kiasi cha Dola 4 milioni huku mshindi wa pili akipata kitita cha Dola 2 milioni na timu mbili zinazoishia hatua ya nusu fainali kila moja inapata kiasi cha Dola 1.2 milioni.

Baada ya mechi za kwanza za hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kumalizika kwa sare tasa wiki iliyopita, timu mbili zitakazokutana kwenye fainali zitapatikana leo.

Mchezo wa kwanza utaanza saa 1:00 usiku katika Uwanja wa kimataifa wa Cairo, Misri ambayo itakutanisha wenyeji Al Ahly dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Saa mbili baadaye, Pyramids FC itakuwa katika Uwanja wake wa nyumbani wa Juni 30, jijini Cairo ambapo itaikaribisha Orlando Pirates nayo ikitokea Afrika Kusini.

Ni mechi za mtego kwa timu zote nne kutokana na aina ya matokeo ambayo kila moja ili isonge mbele baada ya miamba hiyo kushindwa kufungana katika mechi zilizochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wenyeji wanahitaji ushindi tu ili wasonge mbele lakini wageni wao wanaweza kutinga fainali kwa kupata ushindi au sare ya mabao  na iwapo mechi hizo zitamalizika kwa sare tasa kama ilivyokuwa katika michezo iliyopita, washindi watapatikana kwa mikwaju ya penalti.

Kocha wa Al Ahly, Marcel Kohler amesema kuwa wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono.

"Katika mechi ya kwanza, hakuna timu iliyoweza kufunga, kwa hivyo tunatarajia mechi itakuwa na ushindanii sana. Hata hivyo, tutacheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu, ambao watajaza viti.

"Tunawaomba mashabiki kuanzia dakika ya kwanza hadi dakika ya mwisho ya mechi. Waisaidie timu kufanya vizuri zaidi. Lengo letu ni kufika fainali, na tutafanya kila tuwezalo kufanikisha hilo," amesema Kohler.

Kocha wa Miguel Cardoso amesema kuwa hawana presha ya kucheza ugenini dhidi ya Al Ahly na anaamini kwamba watapata matokeo mazuri mbele ya mashabiki wa wapinzani wao.

"Tunajisikia kuwa na nguvu zaidi na tutegemee tunaweza kunyamazisha umati wote. Wanapotuzomea au kutupigia miluzi, ina maana kwamba tunafanya vizuri. Lakini hilo ndilo tunaloishi maisha yetu, kwa muda kama huu.

Kwa hakika, tutakuja na shauku kubwa na si kwa aina yoyote ya hofu kuhusu watu," amesema Cardoso.