Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe atwaa kiatu cha dhahabu Ulaya akiweka rekodi

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Mbappe ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza akiwa na jezi ya Real Madrid ukiwa ni mwanzo mzuri wa kutimiza ndoto zake za kubeba Ballon d'Or.

Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe ameandika rekodi mpya katika historia yake ya soka baada ya kushinda tuzo ya mfungaji bora wa Ulaya. Mbappe amefunga jumla ya mabao 31 katika msimu huu kwenye Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ akiwa ndiye kinara kwa ufungaji mabao katika ligi tano bora Ulaya.

Kwa kufunga mabao hayo 31, Mbappe atapata kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa jumla Ulaya pamoja na kile cha Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’.

Licha ya mshambuliaji wa Sporting CP ya Ureno, Viktor Gyokeres kufunga mabao 39 kwenye ligi hiyo lakini bado Mbappe anampiku kwa sababu mchezaji anapofunga bao kwenye zile ligi tano bora Ulaya yaani Ligi Kuu England (EPL), La Liga, Seria A, Bundesliga na League One bao moja huwa linakuwa na pointi mbili kwa mchezaji.

Kwa maana hiyo, Mbappe ambaye amefunga mabao 31 kwenye La Liga amekuwa na pointi 62 tofauti na Gyokeres ambaye amekuwa na pointi 58.5. Mbali na Gyokeres, Mbappe amemshinda pia mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ambaye amemaliza msimu akiwa amefunga mabao 29.

Nyota huyo raia wa Ufaransa ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza tangu alipofanya hivyo Mfaransa mwenzake Thierry Henry ambaye alichukua mara mbili mfululizo mwaka 2004 na 2005 alipokuwa na Arsenal.

Mbappé alijiunga na Real Madrid mwanzoni mwa msimu huu wa 2024-2025, akitokea PSG kwa uhamisho wa bure, lakini thamani yake imeonekana wazi uwanjani kwani katika msimu wake wa kwanza akiwa na Los Blancos, ameweka historia mpya baada ya kucheza mechi 55, katika mashindano yote na kufunga mabao 42.

Katika msimu huu, Mbappe amevunja baadhi ya rekodi akiwa Madrid ambapo amevunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Alfredo Di Stéfano ambaye alifunga mabao 27 katika msimu wake wa kwanza wakati yeye akifunga 31.

Pia nyota huyu aliingia kwenye rekodi ya kufunga mabao matatu yaani ‘hat trick’ katika mchezo wa El Clasico unaozikutanisha Barcelona na Real Madrid. Mbappé ameivuka rekodi ya mabao 33 iliyowekwa na Cristiano Ronaldo katika msimu wake wa kwanza wa 2009-2010 alipojiunga na Madrid kutokea Manchester United.