Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United inavyojisuka upya

Muktasari:

  • Beki huyo ambaye tangu awali ilielezwa kuwa hakuwa kwenye mipango ya kocha wa United Eric Ten Hag ameuzwa kwa kitita cha pauni 15 milioni.

Manchester, England. Manchester United, imefikia makubaliano ya kumuuza beki wake Aaron Wan Bissaka kwenda kwenye kikosi cha West Ham.

Beki huyo ambaye tangu awali ilielezwa kuwa hakuwa kwenye mipango ya kocha wa United Eric Ten Hag ameuzwa kuwa kitita cha pauni 15 milioni.

Staa huyo anayecheza upande wa kulia alifanya vipimo vya afya juzi lakini jana jioni ndiyo mambo mengi yalitarajiwa kukamilika kutokana na dili hilo.

Hata hivyo, United wanaweza kukamilisha usajili wa wachezaji wawili muda wowote kuanzia leo ambapo watamchukua  Matthijs de Ligt na Noussair Mazraoui kutoka kwenye kikosi cha Bayern Munich ambao wote jana walikula chakula cha usiku kwenye jiji la Manchester.

Mazraoui dili lake linatajwa kukamilika mara baada ya Wan-Bissaka kuuzwa, lakini pia inataka kumchukua Mario Hermoso  ambaye ameachana na Atletico Madrid.

Hata hivyo, United imekubaliana na kiungo Bruno Fernandes kuwa ataongeza mkataba mwingine wa kusalia klabuni hapo baadaye mwezi huu.

Wan-Bissaka alifanikiwa kuichezea United michezo 190, akifunga mabao mawili tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2019 akitokea Crystal Palace  kwa kitita cha  pauni 50 milioni.

Huu umekuwa usajili wa saba wa West Ham msimu huu ikiwa inatarajiwa kuwa na kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu England chini ya kocha Julen Lopetegui.

Timu hiyo imefanikiwa kuwanasa Max Kilman, Niclas Fullkrug, Crysencio Summerville, Luis Guilherme, Wes Foderingham na Guido Rodriguez ambao wameigharimu timu hiyo zaidi ya pauni 100 milioni.

United yenyewe itatakiwa kutoa kitita cha pauni 17 milioni kwa ajili ya kumchukua  Mazraoui akiwa ndiye mbadala wa Wan-Bissaka ambapo pauni 13 milioni zitalipwa mwanzo na  pauni 4 milioni baadaye.

Beki huyo mwenye miaka 26 ambaye amewahi pia kuichezea Ajax chini ya kocha Erik ten Hag amebakiza mkataba wa mwaka mmoja tu kwenye kikosi cha Bayern.

Usajili huu unafanyika siku chache kabla Ligi Kuu England haijaanza wikiendi ijayo.