Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo mawili Sowah kwenda Simba

Muktasari:

  • Singida wamepata hela zinaweza kuwasaidia kujitoa kwenye adhabu ya FIFA, lakini pia wamefanikiwa kusafisha jina lao.

Jonathan Sowah, mshambuliaji hatari zaidi kwenye ligi yetu kwa msimu uliopita, ametimkia Simba SC.

Sowah alisaini Simba SC jioni ya Jumanne ya Julai 22, mwaka huu na kumfanya awe sehemu ya kikosi cha Simba cha msimu ujao.

Sowah ni mshambuliaji bora sana, kwa namba na sanaa ya mpira, hivyo ni sahihi kusema Simba wamepata mshambuliaji hasa.

Alijiunga na Singida Black Stars kwenye usajili wa dirisha dogo la Januari 2025 akitokea Al Nasr ya Libya.

 Amecheza mechi 14 na kufunga mabao 13, hii sio ya kupuuza hata kidogo.

Unaweza kudhani angekuwa na mabao mangapi endapo angeanza msimu akiwa Singida Black Stars?


SASA NI MALI YA SIMBA

Msimu ujao, Sowah atakuwa akivaa jezi nyekundu na nyeupe za Simba na ataanza tangu mwanzo wa msimu.

atakuwa kwenye timu inayoshambulia zaidi ya Singida Black Stars. Atakuwa kwenye timu inayopata faida ya makosa ya kibidamu ya waamuzi zaidi ya Singida Black Stars. Na atakuwa kwenye timu yenye mashabiki wengi zaidi ya Singida Black Stars.

Hii inatoa picha kwamba yawezekana na yeye akawa wa moto zaidi ya alivyokuwa Singida Black Stars.

Lakini hata hivyo, jiulize kwanini Singida Black Stars wamuachie mchezaji bora kama huyu ilihali na wao ni washindani kwenye ligi na pia wanataka kufanya vizuri kimataifa?

Ni kwamba kuna misukumo miwili kutoka nje ya klabu hiyo imemtoa Sowah kwao; madeni na siasa.


MADENI

Singida Black Stars inadaiwa na wachezaji wengi sana na inaweza kufungiwa na FIFA kufanya usajili, kama mambo hayatakuwa sawa.

Huu ni ugonjwa unaoitafuna sana klabu hiyo tangu enzi za Singida United, Singida Big Stars, Singida Fountain Gate na sasa Singida Black Stars.

Unaweza timu zote hizi ni taasisi moja kwa sababu ya watu wanaoonekana kila siku.

Ramadhan Nswanzurwimo na Muhibu Kanu wapo tangu enzi za Singida United.

Hussein Massanza yupo tangu enzi za Singida Big Stars.

Kuna uwezekano mkubwa kabisa kwamba timu hizi ziko chini ya mwamvuli mmoja na ndio maana watu ni wale wale na tatizo sugu ni lilelile.

Julai 25 taarifa kutoka FIFA zilisema klabu hiyo imefungiwa kufanya usajili wa wachezaji wapya hadi ilipe madeni ya wachezaji wao wa zamani.

Inasemekana wachezaji wao kama Faria Odongo na Amade Momade ndio waliofungua kesi.

Katika kuhangaika na madeni haya, Singida Black Stars imeona itumie rasilimali walizonazo ili kujinusuru.

Tayari walishamuuza 'Mtanzania' Josaphat Arthur Bada kwenda JS Kabylie ya Algeria, na sasa wamemuuza Jonathan Sowah kwenda Simba.

Na bado kuna mpango wa kumuuza Mohamed Damaro, fundi mwingine kwenye kiungo cha chini.


SIASA

Kuuza mchezaji sio tatizo, tatizo umemuuza kwa nani?

Mpira wa Tanzania una mambo mengi sana.

Kuna pande mbili ambazo watu wanalazimishwa kuwepo, watake wasitake.

Pande hizo na Simba na Yanga. Yaani kila mtu anatakiwa awe Simba au Yanga, hata ujitetee vipi, hakuna atakayekuelewa.

Na katika hilo, Singida Black Stars wamewekwa upande wa Yanga.

Tangu enzi za Singida United japo timu hiyo huko nyuma ilikuwa ya Mo Dewji, ambaye anajulikana kuwa na Simba damu.

Lakini ujio wake kwenye ligi kuu msimu wa 2017/18, ikiwa na kigogo ambaye ni Yanga wa kutupwa, ukaiweka upande wa njano na kijani.

Na kitendo cha kigogo huyo kumtoa mchezaji wake, Feisal Salum na kumpeleka Yanga mwaka 2018, kikaongeza mafuta kwenye moto.

Hakuna aliyejisumbua kujua chochote pale Kennedy Juma alipotoka Singida kwenda Simba 2019, tayari watu walishakuwa na majibu yao.

Sasa hayo majibu ndio yamekuwa yakiitesa Singida kila uchao.

Katika kuhangaika na jinamizi hili, kigogo huyo alishawahi kusema kwamba aliwapa Simba Aishi Manula.

Kama ni kweli ama si kweli, anajua yeye na mchezaji mwenyewe lakini hata hivyo, hiyo haikusaidia.

Singida ikifungwa tu na Yanga watu hawajadili mpira, wanajadili Singida tawi la Yanga.

Simba imefungwa mechi tano mfululizo na Yanga ndani ya misimu miwili iliyopita, lakini hakuna anayesema Simba ni tawi la Yanga japo Simba imetokana na Yanga.

Ila timu nyingine ikifungwa mfululizo namna hiyo, itaitwa tawi...kwamba wanaachia tu.

Singida Black Stars ilipofungwa na Yanga 2-1 kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu, kelele zilikuwa hizo hizo.

Sasa katika kujisafisha na siasa hizi chafu, Singida ikaona bora ifanye biashara na Simba ili ionekane haibagui.

Sowah angeweza kuuzwa klabu nyingine yoyote, hata Yanga...ikizingatiwa yeye mwenyewe alishawahi kutamka kwamba Rais wa Yanga,  Hersi Said, ni kama baba yake.

Lakini kwenda kwake Simba kuna faida kubwa sana kisiasa kwa Singida Black Stars.

Singida wamepata hela zinaweza kuwasaidia kujitoa kwenye adhabu ya FIFA, lakini pia wamefanikiwa kusafisha jina lao.

Na endapo Sowah atawaka Simba, Singida watapata pa kusafishia zaidi.

Hongera Singida Black Stars kwa kuzicheza karata zenu vizuri.

Hongera Simba kwa kupata mchezaji mzuri.