Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mainoo anataka kusepa jumla

Muktasari:

  • Staa huyo anataka kuondoka jumla kwenda kujiunga na timu zitakazompa nafasi ya kucheza ili kuweka hai matumaini ya kuwamo katika kikosi cha England

Manchester, England. Kiungo Kobbie Mainoo ameripotiwa kuwa anapiga hesabu za kutaka kuachana jumla na klabu yake ya sasa ya Manchester United.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 20 anataka kuachana na miamba hiyo ya Old Trafford kutokana na kukosa nafasi ya kucheza chini ya kocha Mreno, Ruben Amorim.

Mainoo ameanzishwa katika mechi moja tu msimu huu wakati Man United ilipokutana na udhalilishaji mkubwa wa kufungwa na timu ya daraja la chini, Grimsby Town kwenye Kombe la Ligi kwa penalti 12-11 baada ya dakkika 120 kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, Agosti 27 mwaka huu.

Staa huyo alilazimisha kuondoka kwa mkopo mwishoni mwa msimu uliopita katika dirisha la majira ya kiangazi, lakini klabu ya Man United iligoma kumruhusu na kuisalia kikosini hadi sasa akiendelea kuwa mtazamaji mara nyingi au kuanzia benchi.

Amorim alitarajia kumpanga Mainoo katika mechi ya Aston Villa, Jumapili iliyopita, lakini alipata majeraha mazoezini na kumfanya akose pia mechi iliyofuatia ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle United, Ijumaa iliyopita.

Kutokana na dirisha la uhamisho la Januari likibakiza siku chache tu kufunguliwa, Mainoo ameibuka upya na mpango wa kutaka kuondoka, lakini safari hii isiwe kwa mkopo.

Staa huyo anataka kuondoka jumla kwenda kujiunga na timu zitakazompa nafasi ya kucheza ili kuweka hai matumaini ya kuwamo katika kikosi cha England kitakachokwenda kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika kwenye nchi za Marekani, Canada na Mexico.

Napoli ya Italia ni miongoni mwa timu zinazohitaji saini ya mchezaji huyo, ambako kama dili litatiki basi atakwenda kukutana na wachezaji wenzake wa zamani wa Old Trafford, kiungo Scott McTominay na mshambuliaji Rasmus Hojlund kukiwasha katika Serie A.

Hata hivyo, Man United itashawishika kumuuza Mainoo kama tu itapokea ofa ya pesa ndefu kwa sababu kwa sasa ina pengo kubwa katika safu ya kiungo.

Bruno Fernandes ni majeruhi na Casemiro amemaliza dakika 90 katika mechi tatu tu za Man United kwa msimu huu. Kinyume cha hapo, Man United itamruhusu Mainoo kuondoka kama itawapata viungo inaowasaka, ambapo katika mipango iliyonayo kwa Elliot Anderson, Carlos Baleba na Adam Wharton.

Man United leo Jumatatu inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Old Trafford kuvaana na Wolves katika mechi ya Ligi Kuu England kuanzia saa 5:15 usiku.