Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madeni ya Aziz Ki Kariakoo Dabi

Muktasari:

  • Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 58 ilizopata katika mechi 22 na Simba inashka nafasi ya pili na pointi 54 ilizokusanya katika mechi 21.

Kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki ametoa ahadi ya kumpa zawadi, Waziri wa Madini na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Klabu hiyo, Anthony Mavunde katika siku ya mchezo wao dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Machi 8 mwaka huu kuanzia saa 1:15 usiku.

Hilo sio jambo geni kwa Stephane Aziz Ki kwani amewahi pia kumuahidi Mavunde kuwa angefunga bao katika mechi yao dhidi Simba, Aprili 20, 2024 na mchezaji huyo akafanya hivyo kwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-1 ambao Yanga iliupata siku hiyo.

Hata hivyo ahadi aliyotoa kwa Waziri Mavunde ni mojawapo tu kati ya madeni ambayo mchezaji huyo anapaswa kuyalipa kupitia mchezo wa 'Kariakoo Derby' utakaozikutanisha timu hizo mbili Jumamosi hii ambao kwa upande mwingine umeshikilia hatima ya ubingwa kwa miamba hiyo ya soka nchini.


Deni la Iddi Moshi 'Mnyamwezi'

Hii ni mechi ya kwanza kuzikutanisha Yanga na Simba baada ya Stephane Aziz Ki kumuoa mwanadada Hamisa Mobetto na ikiwa atafunga bao, atafuata historia ya nyota wa zamani wa Yanga, Iddi Moshi.

Agosti 5, 2000, Iddi Moshi aliiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba ambapo yeye alifunga mabao yote hayo, akifanya hivyo akiwa ametoka kufunga ndoa huko Tabora.

Kabla na baada ya hapo hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kufanya hivyo na fursa hiyo imetua kwa Aziz Ki ambaye anaweza kuitumia vyema kufuata nyayo za Mnyamwezi au asiweze.


Deni la mabao 14

Msimu uliopita Stephane Aziz Ki aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu baada ya kufumania nyavu mara 21.

Amebakiza mabao 14 ili aweze kufikia rekodi yake ya msimu uliopita lakini amebakiza mabao matatu kuwafikia Clement Mzize, Prince Dube na Charles Ahoua ambao wanaongoza chati ya kufumania nyavu kwenye Ligi Kuu msimu huu, kila mmoja akipachjika mabao 10.

Kufunga dhidi ya Simba kutakuwa na maana kubwa kwa mchezaji huyo katika harakati zake za kutimiza malego hayo mawili.