Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool, Arsenal zapewa saizi yao Carabao Cup

Muktasari:

  • Katika timu 16 zilizobaki, 11 ni za Premier League huku zingine zikitokea madaraja ya chini ikiweno Grimsby Town inayoshiriki Ligi Daraja la Nne, ikiwa ndio ya chini zaidi iliyosalia.

Droo ya hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Carabao, imepangwa usiku wa kuamkia leo huku timu za Arsenal, Newcastle, Liverpool na Wolves zikianzia nyumbani kucheza dhidi ya wapinzani wao wa Premier.

Katika timu 16 zilizobaki, 11 ni za Premier League huku zingine zikitokea madaraja ya chini ikiweno Grimsby Town inayoshiriki Ligi Daraja la Nne, ikiwa ndio ya chini zaidi iliyosalia. Itacheza dhidi ya Brentford ya Premier.

Grimsby haijafika hapo kwa bahati mbaya kwani imeitoa Manchester United na Sheffield Wednesday.


Wakati wa kuisaka hatua hiyo ya 16 bora, Liverpool iliyopoteza fainali ya msimu uliopita mbele ya Newcastle United, imefuzu baada ya Jumanne wiki hii kuichapa Southampton mabao 2-1, huku Chelsea nayo ikisonga mbele kwa ushindi kama huo dhidi ya Lincoln inayoshiriki League One.


Siku ya Jumatano, Manchester City imeichapa Huddersfield 2-0 na Arsenal pia imeibuka mbabe mbele ya Port Vale kwa ushindi kama huo.


Bingwa mtetezi, Newcastle imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Bradford City, huku Brighton ikiinyuka Barnsley mabao 6-0.


Katika droo iliyochezeshwa, Cardiff City iliyoshinda ubingwa wa michuano hiyo mwaka 2012, inakabiliwa na safari ya kwenda kucheza dhidi ya Wrexham wakati Arsenal, Liverpool na Chelsea zote zikiwa zimepangwa dhidi ya wapinzani wenzao wa Premier ambazo ni Brighton, Crystal Palace na Wolves.


Mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Crystal Palace unaturudisha nyuma kidogo wakati timu hizo zilipokutana katika Ngao ya Jamii msimu huu na Crystal Palace kushinda kwa penalti 3-2 baada ya dakika tisini matokeo kuwa sare ya mabao 2-2.


Kabla ya mchezo huo wa Carabao, wikiendi hii Liverpool itakuwa mwenyeji wa Crystal Palace kwenye Premier.


Mechi zingine ni Swansea ya Championship itakabiliana na Manchester City na Wycombe League One itaikaribisha Fulham.


Bingwa mtetezi, Newcastle, unaweza kusema inakabiliwa na mtihani mgumu zaidi itakapoikaribisha Tottenham kwenye Uwanja wa St. James’ Park.


Ratiba kamili ya mechi za hatua ya 16 bora zitakazochezwa Oktoba mwaka huu ipo hivi:

Arsenal v Brighton

Grimsby Town v Brentford

Swansea City v Man City

Newcastle v Tottenham

Wrexham v Cardiff City

Liverpool vs Crystal Palace

Wolves v Chelsea

Wycombe v Fulham