Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao la van Dijk lamtibua Simeone Ligi ya Mabingwa Ulaya

Muktasari:

  • Bao hilo la dakika za jioni liliamsha hasira za kocha Diego Simeone, aliyelazimika kuondoka uwanjani kwa amri ya mwamuzi

Liverpool, England. Liverpool imeendeleza tabia yake ya kupata ushindi katika dakika za majeruhi baada ya Virgil van Dijk kufunga kwa kichwa dakika ya 92 na kuipa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Atletico Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, usiku wa jana.

Bao hilo la dakika za jioni liliamsha hasira za kocha Diego Simeone, aliyelazimika kuondoka uwanjani kwa amri ya mwamuzi baada ya kugombana na mashabiki waliokuwa wakimzomea.

Hii ni mara ya tano mfululizo msimu huu kwa mabao ya ushindi ya Liverpool kupatikana katika dakika za nyongeza (88, 100, 83, 95 na sasa 92), jambo linalomfanya kocha Arne Slot kuhusishwa na matukio ya dakika za mwisho Anfield.

Mo Salah na Andrew Robertson waliwasha moto kwa kufunga mabao mawili ya mapema ambapo hali ilionekana kama Liverpool ingeweka kapuni ushindi mkubwa lakini Marcos Llorente aliibua matumaini kwa Atletico kwa kufunga bao la kwanza sekunde chache kabla ya mapumziko.

Llorente alirudi tena kipindi cha pili na kupiga shuti lililomgonga Alexis Mac Allister kabla ya kujaa wavuni, na kumfanya Simeone kurukaruka uwanjani kana kwamba ameshinda bahati nasibu.

Lakini furaha yake haikudumu baada ya Van Dijk kupaa juu ya mabeki na kutikisa nyavu upande, bao lililogeuza usiku kuwa sherehe ya Majogoo wa Anfield.

Mechi nyingine zilizochezwa jana ilishuhudiwa Bayern Munich ikiichapa Chelsea mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Alianz Arena, Ujerumani.

Mabao ya Bayern yalifungwa na Trevoh Chalobah katika dakika ya 20 kabla ya Harry Kane kuzamisha mabao mawili wakati bao la kufutia machozi kwa upande wa Chelsea likifungwa na Cole Palmer.

PSG ilipata ushindi wa mabao 4-0 ikiichapa Atalanta ya Italia wakati Ajax ikikubali kipigo cha mabao 2-0 ikiwa nyumbani dhidi ya Inter Milan.

Slavia Prague ilitoshana nguvu na Bodo/Glimt kwa kufungana mabao 2-2 huku Olympiacos Piraeus na Pafos zikitoka suluhu.

Mechi nyingine za Ligi ya Mabingwa Ulaya zitachezwa tena leo ambapo Newcastle United itakuwa nyumbani dhidi ya Barcelona, Manchester City wataikaribisha Napoli kwenye Uwanja wa Etihad wakati Bayer Leverkusen watakuwa wageni wa Copenhagen.

Club Brugge itakuwa nyumbani dhidi ya Monaco, Eintracht Frankfurt watacheza na Galatasaray huku Sporting CP wataikaribisha Kairat Almaty ambayo inashiriki Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza.