Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kompyuta yaikataa Liverpool kutinga Ligi ya Mabingwa Ulaya

Muktasari:

  • Liverpool inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Englnd ikiwa imekusanya idadi ya pointi 48 katika mechi 29.

Mfumo wa Kompyuta wa mtandao wa Opta unaotumika katika ubashiri wa soka, umeipa nafasi finyu Liverpool kumaliza katika nafasi nne za juu katika Ligi Kuu ya England (EPL) msimu huu ambazo timu zinazomaliza hapo zinafuzu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Timu zilizopewa nafasi kubwa kumaliza katika nafasi nne za juu kwa mujibu wa ubashiri wa Opta ni Arsenal, Man City, Aston Villa na Man United.

Kwa mujibu wa Opta, Aston Villa ina nafasi ya asilimia 80 kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, mbele ya Manchester United ambayo imepewa nafasi ya asilimia 76.2.

Kwa upande wa Chelsea, takwimu zinaonyesha wana uwezekano wa asilimia 65.7 kumaliza katika nafasi tano za juu.

Nafasi hiyo inatarajiwa kuwa ya kutosha kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kiwango kikubwa cha alama za UEFA ambacho England imekusanya.

Hata hivyo, Liverpool wanaonekana kuwa katika hatari ya kukosa tiketi ya mashindano hayo kwa mujibu wa tathmini ya kompyuta maalum ya uchambuzi wa takwimu ya Opta inayowapa nafasi ya asilimia 63.1 tu kufanikiwa.

Brentford ndiyo inayowakaribia zaidi vigogo hao wanne, lakini ina nafasi ndogo ya asilimia 10.8 tu kumaliza katika nafasi tano bora.

Timu nyingine zinazofuata kwa mbali ni Everton, Newcastle United na AFC Bournemouth.