Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Azam atangaza vita nne bora

AZAM Pict

Muktasari:

  • Azam itakuwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Kagera kukabiliana na wenyeji, ikiwa imetoka kupoteza mechi mbili mfululizo, huku kocha akisema hawataki kurudia makosa.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Rachid Taoussi amesema bado hajakata tamaa ya kupambana kumaliza ndani ya Nne Bora ya Ligi Kuu na kwa sasa anarejea tena katika vita ya ligi hiyo kwa kukabiliana na Kagera Sugar ugenini ili kujiweka pazuri.

Azam itakuwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Kagera kukabiliana na wenyeji, ikiwa imetoka kupoteza mechi mbili mfululizo, huku kocha akisema hawataki kurudia makosa.

Taoussi amesema licha ya kutoka kupoteza mechi mbili mfululizo, lakini bado ameridhishwa na uwezo wa wachezaji katika mazoezi na hatarajii kurudia makosa kimbinu hata kwa wachezaji wenyewe kwani wanaisaka nafasi ya uwakilishi kimataifa.

“Tumekuwa na maandalizi mazuri na kama nilivyosema tangu awali malengo yetu ni kuendelea kushikilia nafasi tuliyopo na ikiwezekana tuzidi kusogea juu walipo wapinzani wetu, hakuna kilichobadilika zaidi ya morali kwa wachezaji wangu,”  alisema Taoussi.

Aliongeza, jambo zuri ndani ya timu hiyo ni wachezaji kubaini makosa waliyoyafanya kwenye mechi zilizopita wakiruhusu kufungwa mabao matatu wao wakifunga moja tu na kupoteza pointi sita muhimu.

“Hali ya kikosi kwa sasa ni nzuri na hakuna taarifa ya majeraha mapya, tunaenda ugenini kutafuta pointi tatu ili kuirudisha timu kwenye morali na pia kuongeza mlima kwa timu inayotukimbiza.”

Azam itapambana na Kagera inayojitafuta msimu huu, huku rekodi zikionyesha mara ya mwisho zilipokutana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Azam ilishinda kwa bao 1-0 Novemba 23, mwaka jana. Bao hilo pekee likifungwa kwa penalti na Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Katika mechi 26 ilizocheza Azam hadi sasa katika Ligi Kuu imeshinda 15, sare sita na kupoteza mechi tano ikikusanya pointi 51 nyuma pointi 16 na kinara wa ligi Yanga, lakini ikiwa imeondoshwa pia kwenye michuano ya Kombe la TFF hivyo tiketi ya kufuzu CAF ni kumaliza katika nafasi ya tatu.