Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa kichapo Brazil yalia na Waamuzi, Polisi

Timu ya taifa ya Brazil, imehitimisha kampeni yake ya kufuzu Kombe la Dunia kwa aibu baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 mbele ya Bolivia katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa El Alto ambao upo mita 4,150 juu ya usawa wa bahari.

Kichapo hicho kimeifanya Brazil kumaliza nafasi ya tano ikiwa na alama 28 katika michezo 18 iliyocheza, rekodi ambayo ni mbaya zaidi katika historia yao ya kufuzu.

Bao pekee la mchezo liliwekwa kimiani kupitia mkwaju wa penalti baada ya Bruno Guimarães kumchezea rafu mshambuliaji wa Bolivia sekunde za mwisho kabla ya mapumziko.

Wenyeji walishangilia kama wamefuzu fainali, huku Brazil wakionekana hoi na kukosa mbinu za kurudi mchezoni licha ya Carlo Ancelotti kuwatupa dimbani nyota kama Marquinhos, Raphinha na kinda Estevão.

Rais wa Shirikisho la Soka Brazil (CBF), Samir Xaud, alifunguka kwa hasira baada ya filimbi ya mwisho, akiwalalamikia kila mtu kuanzia waamuzi, polisi hadi wavulana wa kurusha mipira (Ball Boys).

“Tulikuja kucheza mpira, lakini tulikuta mchezo wa ajabu kabisa. Tulicheza dhidi ya refa, polisi na hata wavulana wa mipira walikuwa wakitupa mipira ovyo ili kutuvuruga. Hii si hadhi ya soka la kimataifa,” alisema Xaud kwa masikitiko.

Aliongeza kuwa mazingira ya uwanjani yalikuwa mabaya kupita kiasi: “Nilihisi kama tunacheza na wachezaji 14 uwanjani. Hii ni fedheha, na tunataka CONMEBOL ichukue hatua.”

Suala la polisi pia lilizua gumzo, kwani viongozi wa Brazil walidai maafisa usalama walikuwa wakali kupita kiasi kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Rodrigo Caetano, mratibu mkuu wa timu, naye hakuwa nyuma: “Bolivia wamepambana, lakini huu mchezo ulikuwa kama michezo mingine kabisa. Malalamiko hayana nguvu kubwa, lakini haya yaliyotokea hayawezi kupuuzwa.”

Kwa bahati, Brazil wameokolewa na mfumo mpya wa fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazoshirikisha timu 48, ambapo Amerika Kusini imetengewa nafasi sita za moja kwa moja. Hivyo basi, nafasi yao ya tano imewapa tiketi bila jasho la mechi ya mchujo.

Hata hivyo, pamoja na uhakika wa kushiriki fainali na nafasi yao ya juu kwenye viwango vya FIFA, mashaka juu ya ubora wa Brazil yamebaki pale pale.