Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ancelloti aweka rekodi kuwa kocha Brazil

Muktasari:

  • Ancelotti ni kocha wa kwanza kuwahi kushinda mataji katika Ligi tano bora za Ulaya akifanya hivyo katika Ligi ya Serie A (Italia), Ligi Kuu England (EPL), Ligue 1 (Ufaransa), Bundesliga (Ujerumani), na La Liga (Hispania).

Rio de Janeiro. Shirikisho la Soka nchini Brazil (CBF) limemtambulisha Carlo Ancelotti kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil tayari kuanza jukumu la kuinoa timu hiyo ambapo amesaini dili la mwaka mmoja na mabingwa hao mara tano wa dunia hadi mwaka 2026, baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia litakalofanyika Marekani, Canada pamoja na Mexico.

Kocha huyo raia wa Italia ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuifundisha timu hiyo yenye mafanikio makubwa duniani kwani kabla ya ujio wake timu hiyo ilikuwa ikiongozwa na makocha wazawa. Timu ya taifa ya Brazil ilikuwa chini ya makocha wa muda Ramon Menezes na Fernando Diniz, ambao walikuwa wakikaimu nafasi ya Dorival Júnior, aliyekuwa kocha mkuu ambaye alitimuliwa mwanzoni mwa mwaka huu kufuatia kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Argentina ambacho kiliongeza shinikizo la kutimuliwa kwake.

Ancelotti anatarajiwa kukutana na viongozi wa Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) kabla hajakutana na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza huku macho na masikio ya mashabiki yakielekezwa kwake, wakisubiri kuona iwapo ataweza kuirudisha Brazil katika hadhi yake ya juu kisoka duniani.

Brazil wanaamini kuwa huenda Ancelotti anaweza kuwarudisha katika nchi ya ahadi ambapo mwezi ujao atakuwa na kibarua cha kuwakabili Ecuador na Paraguay katika michezo ya kusaka tiketi ya kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia la 2026.

Kocha huyo ameondoka Real Madrid baada ya msimu huu kumalizika huku nafasi yake ikichukuliwa na Xabi Alonso kocha ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa timu hiyo kwa mafanikio. Licha ya kumaliza msimu huu bila kutwaa taji lolote kubwa Ancelotti bado anabaki kuwa ndiye kocha mwenye mafanikio zaidi Ulaya.

Carlo Ancelotti, mwenye umri wa miaka 65, alithibitisha ubora wake baada ya kupata mafanikio makubwa akiwa na miamba hiyo ya Hispania tangu arejee mwaka 2021, ambapo aliiongoza Madrid kutwaa jumla ya mataji 15.

Mataji aliyobeba Ancelotti ni La Liga mara mbili (2022, 2024), Copa del Rey mara mbili (2014, 2023), Spanish Super Cup mara mbili (2022, 2024) UEFA Champions League mara tatu (2014, 2022, 2024).

Mengine ni UEFA Super Cup mara tatu (2014, 2022, 2024), Klabu Bingwa Dunia mara mbili (2014, 2022) na FIFA Intercontinental Cup mwaka 2024. Hili lilikuwa taji la pili msimu huu wa 2024-2025, baada ya kutwaa UEFA Super Cup mwezi Agosti dhidi ya Atalanta.

Carlo Ancelotti pia ni kocha wa kwanza kuwahi kushinda mataji katika ligi tano bora za Ulaya akifanya hivyo katika Ligi ya Serie A (Italia), Ligi Kuu England (EPL), Ligue 1 (Ufaransa), Bundesliga (Ujerumani), na La Liga (Hispania).