Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kane aibua wasiwasi Bayern Munich

KANE Pict

Muktasari:

  • Mkataba wa Kane huko kwenye kikosi cha Ujerumani utafika tamati majira ya kiangazi 2027, hiyo ikiwa na maana Bayern ama kumwongezea mkataba wake au kukubali kumpoteza bure kabisa.

Munich, Ujeruman. Mtaalamu wa soka la Ujerumani, Raphael Honigstein anaamini Bayern Munich na Harry Kane watalazimika kukutana ili kujadili hatima ya straika huyo raia wa England.

Mkataba wa Kane huko kwenye kikosi cha Ujerumani utafika tamati majira ya kiangazi 2027, hiyo ikiwa na maana Bayern ama kumwongezea mkataba wake au kukubali kumpoteza bure kabisa.

Kane, 32, alijiunga na Bayern dirisha la majira ya kiangazi 2023 akitokea Tottenham Hotspur kwa ada ya uhamisho ya Pauni 82 milioni.

Akiwa na kikosi hicho cha Bayern, alishinda taji lake la kwanza kubwa katika maisha yake ya soka na tangu hapo amevunja rekodi kibao.

Lakini, kuwasili kwa mshambuliaji Nicolas Jackson, kuliibua wasiwasi huenda ukahitimisha zama za mwisho za Kane huko Bayern.

Jackson aliwasili Munich akitokea Chelsea kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili na dili la awali ni la mkopo likuwa na kipengele cha kuhitaji kubeba jumla huko Allianz Arena.

Na Honigstein anaamini mpango wa kumleta Jackson ni mwanzo tu wa kutaka kumbadili Kane, hivyo utatoa nafasi kwa staa huyo wa England kurudi Ligi Kuu England.

Honigstein alisema: "Siyo siri tena watu wa Ujerumani hawamtarajii kabisa Harry Kane kubaki hadi mwisho wa mkataba wake. Nadhani ni wazi Bayern inatazama uwezekano wa kumwondoa kabla ya mkataba huu wa sasa kufika mwisho, 2027.

"Ilikuwa inatafuta mtu wa kuwa mbadala wake au atakayecheza chini yake. Walimhitaji Benjamin Sesko. Walimfuatilia pia Nick Woltemade, lakini wameishia kwa Jackson, huku wakiwa na ulazima wa kumnunua jumla.

"Hii ina maana Bayern inatambua wazi Kane anapaswa kuondoka ndani ya mwaka mmoja au miwili. Lakini, kwa wakati huu ni vizuri huyo atakayeletwa aje kucheza pamoja naye. Kwa sasa hakuna nafasi ya Jackson kumbadili Kane. Atacheza pamoja naye au kumpa Kane muda wa kumpumzika kwenye mechi."

Dirisha la usajili la majira ya kiangazi halikuwa na mafanikio makubwa kwa Bayern. Ilinasa saini ya Jackson, Luis Diaz na Jonathan Tah. Kane aliwahi kubainisha kuhusu ukubwa wa kikosi hicho.

Kane alisema: "Ni wazi ni moja ya timu yenye kikosi kidogo."

Straika Kane amekuwa akihusishwa na mpango wa kurudi kwenye Ligi Kuu England kwenda kufukuzia kuvunja rekodi ya mabao ya muda wote kwenye ligi hiyo, inayoshikiliwa na Alan Shearer.

Kwa sasa, Kane anahitaji mabao 50 tu kuvunja rekodi ya Shearer ya mabao 260 kwenye Ligi Kuu England ili awe kinara wa kufunga wa muda wote.

Hata hivyo, ili hilo litokea ni Bayern ndiyo wenye uamuzi wa mwisho.