Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jackson aachwa njia panda kujiunga Bayern

JACKSON Pict

Muktasari:

  • Jackson, mwenye umri wa miaka 24, alikuwa amepewa ruhusa kuondoka Stamford Bridge baada ya kuonekana hana msaada katika kikosi cha kwanza.

London, England. Nyota wa Chelsea na timu ya taifa ya Senegal, Nicolas Jackson, ameripotiwa kuchukizwa vibaya na kuvunjika kwa mpango wake wa kujiunga na Bayern Munich kwa mkopo, licha ya kuwa tayari alishatua Ujerumani kukamilisha dili hilo.

Jackson, mwenye umri wa miaka 24, alikuwa amepewa ruhusa kuondoka Stamford Bridge baada ya kuonekana hana msaada katika kikosi cha kwanza.

Licha ya klabu kadhaa za Ligi Kuu England kutaka kumsajili, Bayern ndio iliibuka kidedea kwa kufikia makubaliano na Chelsea.

Lakini mambo yalibadilika ghafla. Majeraha aliyoyapata mchezaji mpya wa matajiri hao wa Jiji la London, Liam Delap, kwenye mchezo wa mapema Jumamosi dhii ya Fulham, yaliifanya Chelsea kubadili mawazo na kuamua kumrudisha Jackson, licha ya kuwa tayari walishafanya makubaliano ya ada ya rekodi ya uhamisho wa mkopo ya Pauni 13 milioni na mchezaji kuwa ameshawasili Munich kumaliza dili.

Mkataba huo wa Jackson pia ulikuwa na kipengele cha kumunua mazima mwisho wa msimu huu kwa kutoa Pauni 56 milioni.

Jackson hajaridhishwa na mabadiliko hayo ya dakika za mwisho na sasa yeye pamoja na mawakala wake wanapambana kuhakikisha dili la kusaini Bayern linafanikiwa.

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern, Max Eberl, alizungumza kabla ya mechi dhidi ya Augsburg na kuashiria kuwa bado mambo yanaweza kubadilika:"Usajili unakamilika mara tu pale ambapo kuna saini rasmi. Yuko hapa Jackson, lakini ngoja tuone kitakachofuata. Mara nyingine timu zinakubaliana na mchezaji anafanya vipimo vya afya, kisha mambo ya ajabu hutokea. Kwa sasa siwezi kusema nini kinaendelea."

Hata hivyo, Chelsea inasisitiza kuwa Jackson arejee London na kujiunga tena na kikosi cha kwanza baada ya kuumia kwa  Delap na hadi sasa haijabadilisha msimamo wake.

Awali, Chelsea ilikuwa imewasajili  Delap na Joao Pedro, ikiamini wawili hao ndio watakaobeba jukumu la kufunga mabao baada ya Christopher Nkunku kutimkia AC Milan na Jackson kuruhusiwa kuelekea Bundesliga.

Lakini sasa, baada ya majeraha ya Delap, mpango mzima umevurugika. Jackson anatakiwa kurudilicha ya kocha Enzo Maresca mwezi huu kuashiria wazi kuwa nafasi ya staa huyo wa kimataifa wa Senegal katika kikosi chake ni finyu na ni vyema zaidi akiondoka.

"Ni bora kwa Nico kuondoka kwa sababu hatokuwa sehemu ya kikosi kwani tuna wachezaji wawili kwenye nafasi yake. Akipata  timu ataruhusiwa kuondoka."