Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nicolas Jackson atemwa Chelsea

Straika wa Chelsea, Nicolas Jackson, ameachwa nje ya kikosi kitakachovaana na Bayer Leverkusen kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa leo usiku, huku taarifa zikisema klabu hiyo sasa inamsaidia kupata timu mpya.

Taarifa zinasema Jackson (24) alifanya mazoezi peke yake kwenye kituo cha Cobham leo, wakati wenzake wakijiandaa na mechi ya dhidi ya wababe wa Bundesliga, Bayer Leverkusen.

Msenegali huyo ameshawaambia mabosi wa Chelsea rasmi kuwa anataka kuangalia uwezekano wa kuhamia kwingine msimu huu wa usajili. Klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo na vilabu kadhaa vya England na Ulaya, na wapo tayari kumuuza endapo itakuwa kwa maslahi yao.

Hata hivyo, iwapo hatopata timu hadi dirisha la usajili lifungwe, Chelsea wamesema wataendelea kumhusisha kwenye mipango ya kocha Enzo Maresca, kwani bado wanamwona kama mchezaji muhimu.

Newcastle United ndiyo wanatajwa zaidi kumfuatilia Jackson baada ya kukosa kumchukua Benjamin Sesko wa RB Leipzig, huku pia AC Milan na Juventus wakionyesha nia. Chelsea wanadai thamani yake ni kubwa kuliko paundi milioni 74 walizolipwa Leipzig kwa Sesko na pia paundi milioni 79 ambazo Liverpool waliilipa Eintracht Frankfurt kwa Hugo Ekitike.

Jackson, ambaye ana uzoefu wa Premier League, hata hivyo hatacheza mchezo wa kwanza wa msimu mpya kutokana na adhabu ya kufungiwa mechi moja baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu dhidi ya Newcastle mwezi Mei, kwa kumpiga kiwiko cha usoni beki Sven Botman.