Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jina la Mokwena, kocha Asec yachomoza Yanga

Mabosi wa Yanga, wameendelea kufanya yao kimyakimya katika mchakato wa nani kusaka kocha atakayepewa nafasi ya kuiongoza Yanga kwa msimu ujao umechukua sura mpya baada ya kuamua kuliongeza jina la kocha mmoja kutoka nyumba ya vipaji raia wa Ufaransa.

Yanga ipo katika mipango ya kutemana na Miloud Hamdi anayeionoa kwa sasa ambaye alitua kutoka Singida Black Stars ili kuchukua nafasi ya Sead Ramovic aliyetimkia CR Belouizdad ya Algeria.

Sasa unaambiwa ni kwamba, mezani kwa mabosi wa Yanga kwa sasa kuna majina mawili likibaki la Rhulani Mokwena, lakini akaongezeka Julien Chevalier anayemalizia mkataba alionao pale ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Taarifa za kuaminika ambazo Mwananchi inazo ni kwamba mazungumzo ya Yanga na Mokwena yanaendelea vizuri, huku kocha huyo akiendelea kutoa masharti mbalimbali, lakini changamoto kubwa ni kwamba ofa tofauti zimeendelea kumfuata tangu aachane na Wydad Athletic ya Morocco.

Mokwena anaijua vizuri Yanga na Mwananchi limejulishwa kuwa, kocha huyo anataka mambo machache ya kuboreshwa ikiwemo kutanua benchi la ufundi na kusajiliwa wachezaji anaowataka masharti ambayo mabingwa hao wa kihistoria nchini wanapambana nayo, huku dau lake likiwa la kutisha.

Hata hivyo, mabosi wa Yanga wamekaa mezani pia na kocha Chevalier raia wa Ufaransa baada ya kocha huyo kutangaza kuachana na miamba hiyo ya Ivory Coast.

Chevalier anataka kukabiliana na changamoto mpya baada ya kudumua  miaka minne ndani ya ASEC akizalisha mastaa kibao wakiwemo baadhi waliopita na kuwepo Yanga kama Stephane Aziz KI, Pacome Zouzoua, Yao Kouassi na wengineo waliwahi pia kukipiga Msimbazi.

Yanga inataka mmoja kati ya makocha hao aje mapema nchini kumaliza dili hilo kisha kuanza hesabu za kusuka kikosi kipya kushauri pia juu ya ubora wa wachezaji anaowataka.

"Tunataka kufanya maamuzi mapema ili kocha aje kabla ya ligi kwisha atoe mapendekezo yake ya mwisho ili maandalizi ya msimu ujao yaanze mapema,” alisema bosi huyo wa juu ndani ya Yanga.

Ndani ya makocha hao wawili tutaamua kwenda na mmoja kwa kuwa ukitazama wasifu wao unajieleza wanatufaa, tusubiri maamuzi ya mwisho.”

Mokwena kabla ya kutua Wydad iliyoachana naye hivi karibuni, aliwahi kuinoa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchini humo misimu mitatu mfululizo 2021-2022-2022-2023 na 2023-2024 sambamba na kutwaa ubingwa wa African Football League.

Kwa Chevalier aliyejiunga na ASEC Julai 2019 ameiwezesha kutwaa mataji matatu pia ya Ligi Kuu ya Ivory 2021, 2022 na 2023, Kombe la FA 2023 mwaka ambao pia alitwaa ubingwa Félix Houphouët-Boigny Cup, huku Akiifikisha timu hiyo nusu fainali ya Kombe la Shirikisho msimu 2022-2023, ambao Yanga ilifika fainali na kupoteza kwa kanuni ya bao la ugenini dhidi ya USM Alger ya Algeria kwani timu hizo zilifunga mabao 2-2, Yanga ikipoteza nyumbani 2-1 na kushinda ugenini 1-0.