Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii ndiyo sababu iliyomponza Mourinho Uturuki

MOURINHO Pict

Muktasari:

  • Mreno huyo alionyeshwa mlango wa kutokea, Agosti 29 baada ya mwaka mmoja wa kuinoa timu hiyo huku sababu za kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Istanbul, Uturuki. Rais wa Fenerbahce, Ali Koc amefunguka kuhusu uamuzi wa klabu hiyo kumfuta kazi kocha Jose Mourinho.

Mreno huyo aliyejipachikwa jina la Special One alionyeshwa mlango wa kutokea, Agosti 29 baada ya mwaka mmoja wa kuinoa timu hiyo huku sababu za kuondoshwa na timu hiyo kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, iliposukumwa nje na Benfica kwenye mechi ya mchujo.

Wakati matokeo ya jumla ya 1-0 yakidaiwa kuwa si sababu pekee, Koc alisema juu ya timu ilipoteza mechi hiyo ya mbinu za soka la kujilinda na Mourinho lilidaiwa kuwa chanzo kingine.

Bosi Koc alisema: “Kwanini tumemruhusu Mourinho aondoke? Kulikuwa kuachana kunakoumiza. Uhusiano wetu ulikuwa mzuri na kumleta hapa yalikuwa mafanikio makubwa. Lakini, sasa tulihitaji kucheza soka la kutawala, kufunga mabao 99 na kuvuna pointi 99, hiyo ndio DNA yetu.”

Koc aliongeza: “Kutupwa nje na Benfica halikuwa tatizo. Lakini, namna tulivyotupwa nje hiyo haikubaliki. Tuliona kama soka lile la mdororo la msimu uliopita linaendelea na msimu huu.”

Katika kipindi chake alichokuwa kwenye kikosi hicho, Mourinho ameiongoza Fenerbahce katika mechi 62, ikishinda 37, sare 14 na vichapo 11 na hakushinda taji lolote katika kikosi hicho cha Uturuki.

Mourinho pia hakuwa vizuri sana kwenye ligi ya ndani, ambapo timu yake ilishika nafasi ya pili kwenye ligi na ilishindwa kupata ushindi dhidi ya timu yoyote iliyokuwa kwenye Top Five na ilipoteza mechi zote mbili kwenye ligi na mechi za makombe mengine ya ndani dhidi ya mahasimu Galatasaray.

Mourinho aliripotiwa pia kutibuana na mastaa wa kikosi hicho kama Ismail Yuksek na Irfan Can Kahveci. Hata hivyo, CV ya Mourinho imenoga kwelikweli, akibeba mataji kwenye klabu zote alizopita ikiwamo FC Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid, Manchester United na AS Roma.