Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hawa hapa wanamichezo wa Afrika waliofariki 2024

Muktasari:

  • Wanamichezo hawa walifanya makubwa enzi za uhai wao wakiiwakilisha vizuri Afrika katika mashindano mbali mbali.

Mwaka 2024 umeacha majonzi na simanzi kwa wapenzi wa michezo Barani Afrika baada ya kuwapoteza baadhi ya wanamichezo waliokuwa wakiiwakilisha vyema katika mashindano mbali mbali.

Mwanariadha wa Uganda wa mbio za Marathon, Rebecca Cheptegei alifariki dunia Septemba 5, 2024 wakati akipatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kumwagiwa petroli kisha kuchomwa moto na mpenzi wake Dickson Marangach, huku sababu ikitajwa ugomvi wa mgogoro wa kiwanja pamoja na nyumba.

Cheptegei enzi za uhai wake alishiriki katika mbio za Marathon za Olimpiki Paris Agosti 2024.

Kelvin Kiptum (24) alifariki dunia pamoja na kocha wake, Gervais katika ajali ya gari iliyotokea Februari 11, 2024 eneo la Kaptagat karibu na barabara ya Elgeyo Marakwet-Ravine.

Mwanariadha huyu bado anashiklia rekodi ya dunia kwenye mbio za marathon za kilometa 42 zilizofanyika Chicago, Marekani alipomaliza kwa saa mbili na sekunde 35. Kiptum alitajwa kama mpinzani wa Eliud Kipchoge mmoja wa wanariadha wakongwe nchini Kenya.

Gwiji wa mpira wa kikapu, Dikembe Mutombo, alifariki Septemba 30, 2024 baada ya kusumbuliwa na saratani ya ubongo iliyomtesa miaka miwili.

Mutombo alitajwa kuwa mmoja kati wa wazuiaji bora kuwahi kutokea kwenye Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) alifariki akiwa na umri wa miaka 58, huko Atalanta, Marekani.

Mutombo aliyekuwa ana uraia wa DR Congo na Marekani alishawishi wachezaji wengi wa kizazi hiki kuingia kwenye kikapu.

Katika enzi za uchezaji wake alitumikia timu mbalimbali kwa misimu 18 akichezea Denver, Atlanta, Houston, Philadelphia, New York na New Jersey Nets na pia aliingia katika kikosi cha NBA All Star mara nne. Licha ya ubora na rekodi mbalimbali hakuwahi kushinda taji hata moja la NBA katika maisha ya uchezaji.

Issa Hayatou alifariki dunia Agosti 8, 2024 akiwa na umri wa miaka 77, huku akikumbukwa kama Rais aliyeiongoza CAF kwa miaka mingi zaidi 29, akichukua nafasi hiyo tangu mwaka 1988 hadi alipoondoka 2017.

Mbali na uongozi wake katika michezo, alikuwa ni Bingwa wa mbio kitaifa na mchezaji mpira wa kikapu.

Katika uongozi wake, Agosti 2021, Mcameroon huyu alipigwa marufuku ya mwaka mmoja na FIFA kwa kukiuka kanuni za maadili wakati wa kusaini mkataba mkubwa zaidi kuwahi kutokea barani Afrika na kampuni ya habari ya Ufaransa ya Lagardere mnamo 2016.

Adhabu hiyo ilibatilishwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo mnamo Februari mwaka 2017.

Jacques Freitag, Bingwa wa dunia wa kuruka juu 2003 alipatikana amekufa akiwa na majeraha mengi ya risasi katika makaburi huko Pretoria, Afrika Kusini, Julai 2024, baada ya kutoweka wiki mbili.

Mchezaji huyo aliyefariki akiwa na umri wa miaka 42, alishinda medali ya dhahabu kwenye Mashindano ya Dunia huko Paris kwa kipimo cha 2.35m, na kuwa Mwafrika wa kwanza kushinda taji la dunia.

Haikuwa kifo chake pekee cha kikatili nchini Afrika Kusini mwaka huu, kwani beki wa Kaizer Chiefs, Luke Fleurs aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa na umri wa miaka 24 katika wizi wa gari mwezi Aprili.