Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais wa Fifa amlilia Issa Hayatou

Rais wa Shirikisho la Kimataifa ya Soka (FIFA), Gianni Infantino (kushoto) akizungumza jambo na aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou enzi za uhai wake. Picha na Mtandao

Muktasari:

  •  Rais wa FIFA, Gianni Infantino, ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wake, Issa Hayatou, mwenye umri wa miaka 77.

Dar es Salaam. Rais wa Shirikisho la Kimataifa ya Soka (FIFA), Gianni Infantino ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa shirikiho hilo la Afrika, Issa Hayatou.

Hayatou alifariki dunia jana Alhamisi akiwa na umri wa miaka 77, huku akikumbukwa kama Rais aliyeiongoza CAF kwa miaka mingi zaidi 29, akichukua nafasi hiyo tangu mwaka 1988 hdi alipoondoka 2017.

Infantino ametuma salamu za rambirambi kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiandika: "Nimesikitishwa kupokea taarifa za kifo cha aliyekuwa Rais wa CAF, Makamu wa Rais wa FIFA na Mjumbe wa Baraza la FIFA, Issa Hayatou." Ulisomeka ujumbe wa Infantino na kuendelea; 

"Alikuwa shabiki wa michezo wa soka, alijitolea maisha yake kwa usimamizi wa michezo wa soka.

"Kwa niaba ya FIFA, rambirambi ziende kwa familia yake, marafiki, wafanyakazi wenzake wa zamani na wote wanaomfahamu. Pumzika kwa amani."

Agosti 2021 Hayatou alipigwa marufuku ya mwaka mmoja na FIFA kwa kukiuka kanuni za maadili wakati wa kusaini mkataba mkubwa zaidi kuwahi kutokea barani Afrika na kampuni ya habari ya Ufaransa ya Lagardere mnamo 2016.

Adhabu hiyo ilibatilishwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo mnamo Februari mwaka 2017.