EPL, La Liga na vita ya kimaslahi na Fifa

London,England. Uamuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) kuongeza idadi ya timu shiriki kwenye Klabu Bingwa ya Dunia umeibua hofu kwa Ligi Kuu ya England (EPL) na ile ya Hispania (La Liga), zikiona kama utakuwa na athari hasi kiuchumi lakini pia kushusha hadhi ya klabu zao.

Bodi za Ligi hizo mbili zina wasiwasi kwamba uamuzi huo unaweza kuepelekea kwa idadi ya timu kwenye ligi zao hali inayoweza kusababisha kupungua kwa mapato yatokanayo na fedha za udhamini wa luninga na wadhamini wengine, kupoteza ajira za baadhi ya wachezaji na maofisa wa timu lakini pia nembo ya ligi hizo kupungua thamani na mvuto.

Kupungua kwa mapato yatokanayo na haki za udhamini wa matangazo ya luninga kunaripotiwa kwamba kutatokana na kupungua kwa idadi ya mechi ambayo timu kwenye ligi hizo zinacheza kwa msimu jambo ambalo limeanza kuzua wasiwasi kwa La Liga na EPL ambazo zinataka kuchukua hatua za kuona haziathiriki na mashindano hayo ambayo yataanza Juni 15 na kumalizika Julai 13 mwakani.

Kuna wasiwasi kwamba Fifa itatoa amri ya kupunguzwa kwa idadi ya timu mbili kwenye ligi ambazo zinashirikisha timu 20 na hivyo kuzifanya zibakie na timu 18, uamuzi ambao EPL na La Liga zimeibuka hadharani na kuupinga kabla hata haujaripotiwa rasmi au kuanza kutumika.

Rais wa La Liga, Javier Tebas alisema kuwa Fifa inapaswa kukutana na bodi yao na ile ya Ligi Kuu ya England kujadili na kutafuta suluhisho la namna mashindano hayo ya Klabu Bingwa ya dunia yatakavyochezwa ili kutoathiri ligi zao.

"Kama tusipochukua hatua, kiwanda hiki kipo hatarini kwa sasa. Suluhisho la Fifa ni kuanzisha mashindano mapya. Lakini hilo hili litokee na kwa sisi ili tuweze kuwa tayari kuwepo kwenye mashindano hayo ni tunatakiwa kupoteza timu mbili kwenye La Liga.

"Hii inamaanisha kwamba tutawafanya wachezaji 70 kutokuwa na ajira  katika klabu hizo na itapoteza ajira nyingi zihusianazo na klabu husika," alisema Tebas.

Tebas alisema kuwa uamuzi huo utainufaisha Fifa lakini wadau na washirika wake watapata athari kubwa kama kusipokuwepo na utaratibu mzuri wa uwepo wake.

"Tunatakiwa kutatua matatizo kabla hatujaunda mashindano mapya ambayo yataharibu kiwanda hiki, ajira na ndoto za mashabiki na mpira wa miguu," alisisitiza Tebas.

Uchunguzi uliofanywa na bosi wa bodi ya Ligi Kuu ya England, Richard Masters umebaini kuwa tayari uamuzi huo umeshachukuliwa na Fifa na kilichobakia kwa sasa ni utekelezaji wake tu.

Moja ya chanzo cha uhakika kutoka bodi ya Ligi Kuu ya England, kimefichua kwamba amri ya kupunguzwa kwa timu itatangazwa na Fifa hivi karibuni.

"Wote tunafikiria kwamba dhumuni kuu la Fifa ni kutupunguza timu na kubakia 18. Hatuwezi kushtushwa kama tayari wameshaandika hitimisho lao. 

"Unachoweza kuweka pesa zako ni kikundi kazi kusema kuna soka la ndani sana, kwamba sote tunapaswa kushuka kutoka vilabu 20 hadi 18 na kwamba athari ndogo kwa wachezaji inatokana na mechi za kimataifa," kilifichua chanzo hicho.

Ikiwa mpango huo utaanza kufanya kazi, Ligi za England, Hispania, Italia na Ubelgiji ndizo zinaonekana zitaathirika zaidi tofauti na Ujerumani na Ufaransa.

Ligi za England, Hispania na Italia kila moja ina timu 20 na ligi ya Ubelgiji licha ya kuwa na timu 16, timu hulazimika kucheza mechi 10 za mchujo wa kusaka bingwa na timu za kushuka daraja, jambo linalofanya kila timu icheze mechi 40 kwa msimu.

Hadi sasa idadi ya timu 28 kutoka mabara tofauti zimeshafuzu kushiriki mashindano hayo ya klabu bingwa ya dunia mwakani huko Marekani zikingojea timu nne tu zitakazoungana nazo.

Timu hizo zilizofuzu ni Al Hilal, Urawa Red Diamonds, Al Ain, Ulsan HD, Al Ahly, Wydad Casablanca, Esperance, Mamelodi Sundowns, Monterrey, Seattle Sounders, Leon, Palmeiras, Flamengo, Fluminense, River Plate, Auckland City, Chelsea, Real Madrid, Manchester City, Bayern Munich, PSG, Inter Milan, Porto, Benfica, Borussia Dortmund, Juventus, Atletico Madrid na Red Bull Salzbur