Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland kurejea uwanjani leo Man City ikiwa ugenini

Muktasari:

  • Manchester City inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 64.

Wakati ikikaribishwa ugenini na Southampton leo kwenye muendelezo wa Ligi Kuu England (EPL), Manchester City imepata habari njema ya urejeo wa mshambuliaji wake tegemezi, Erling Haaland.

Haaland alikuwa nje ya uwanja tangu Machi akiuguza majeraha ya enka ambayo aliyapata katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Bournemouth, Machi 30, mwaka huu ambao Man City iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Majeraha hayo yalimfanya Haaland akose mechi saba za mashindano tofauti lakini nyota huyo kutoka Norway ka sasa ni mzima na yuko tayari kuitumikia Manchester City katika michezo iliyobakia ya kumalizia msimu ukiwemo wa leo dhidi ya Southampton kwenye Uwanja wa St. Marys.

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa mashabiki wajiandae kumuona Haaland uwanjani leo kwa vile yupo tayari kuitumikia timu hiyo baada ya kupona majeraha yake.

“Yupo tayari, yupo fiti na kama ataanza tutaona kesho (leo),” amesema Guardiola.

Hadi anapata majeraha, Haaland alikuwa amefumania nyavu mara 21 katika mechi 28 za EPL msimu huu na kiujumla amefunga mabao 30 katika mechi 40 za mashindano yote ambayo Manchester City imeshiriki msimu huu huku akipiga pasi nne zilizozaa mabao.

Hata hivyo majeraha ambayo Haaland aliyapata, yameonekana kumuweka katika uwezekano finyu wa kutetea tuzo yake ya mfungaji bora wa EPL msimu huu baada ya kuitwaa kwa misimu miwili iliyopita.

Anayeonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi wa tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu England msimu huu ni nyota wa Liverpool, Mohamed Salah ambaye amefunga mabao 28, saba zaidi ya yale ya Haaland.

Mechi hiyo ya Southampton na Manchester City leo ni miongoni mwa michezo mitano ya EPL ambayo itachezwa leo katika viwanja na miji tofauti England.

Michezo mingine minne ambayo itakuwa leo ni kati ya Fulham na Everton, Ipswich dhidi ya Brentford, Wolves itacheza na Brighton na Bournemouth dhidi ya Aston Villa.


Ratiba ya EPL leo

Fulham vs Everton (Saa 11:00 jioni)

Ipswich vs Brentford (Saa 11:00 jioni)

Southampton vs Man City (Saa 11:00 jioni)

Wolves vs Brighton (Saa 11:00 jioni)

Bournemouth vs Aston Villa (Saa 1:30 usiku)