Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gundogan anukia kurejea Man City

Muktasari:

  • Gundogan (33) aliachana na Manchester City mwaka jana baada ya kuiongoza kutwaa mataji matatu akiwa nahodha.

Manchester, England. Manchester City imeanza harakati za kumrejesha kiungo wake wa zamani, Ilkay Gundogan ambaye anaitumikia Barcelona.

Gundogan (33) aliachana na Manchester City mwaka jana baada ya kuiongoza kutwaa mataji matatu akiwa nahodha.

Barcelona inataka kuachana na mchezaji huyo ili kupisha ujio wa Dani Olmo kwani Gundogan ni miongoni mwa nyota wanaolipwa kiasi kikubwa cha fedha klabuni hapo hivyo kanuni za usajili za Uhispania zinaizuia Barcelona kuingiza mchezaji mpya bila kumuondoa mtu.

Man City inamuona Ilkay Gundogan kama suluhisho la haraka na la muda mfupi katika kutatua upungufu wa wachezaji ambao imekuwa nao katika siku za hivi karibuni.

Upungufu huo umetokana na mauzo ya mshambuliaji Julian Alvarez kwenda Atletico Madrid kwa dau la Pauni 81 milioni lakini pia majeraha ya winga wa Norway, Oscar Bobb.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekuwa akivutiwa na uchezaji wa Gundogan na hata wakati anaondoka alitamani kuona kiungo huyo anabakia kikosini.

Hata hivyo Gundogan aligomea kusalia ndani ya Manchester City kwa vile hakufurahishwa na mkataba wa muda mfupi ambao klabu hiyo ilimpatia ili aendelee kuitumikia ambapo ilimpa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja.

Gundogan alikuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Manchester City kabla hajaondoka na kutimkia Barcelona ambako nako ameonekana kuchemsha.

Baada ya kujiunga na Man City mwaka 2016 akitokea Borussia Dortmund kwa ada ya Pauni 20 milioni, Gundogan alicheza idadi ya mechi 304 za mashindano tofauti kwenye timu hiyo na kuifungia mabao 60.

Katika miaka saba ambayo Gundogan aliitumikia Man City, alitwaa mataji 14 ambapo matano yalikuwa ni ya Ligi Kuu ya England, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya FA, manne ya Calabao na Ngao ya Jamii mara mbili.