Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Edo Kumwembe agundua tatizo la usajili Simba

Mchambuzi mahiri wa soka nchini, Edo Kumwembe amesema kuna tatizo katika idara ya usajili ya Simba, baada ya kuachwa kwa mastaa kadhaa.

Klabu ya Simba imeendelea kuwapa mkono wa kwaheri baadhi ya wachezaji wake huku jambo la kushangaza zaidi ni kuona wachezaji waliojiunga na timu hiyo msimu uliopita nao wakiondoka.

Baadhi ya wachezaji waliopewa mkono wa kwa heri yumo aliyewahi kuwa MVP wa Nigeria msimu wa 2023/2024 Augustine Okejepha, ambaye amedumu kwa mwaka mmoja tu Msimbazi ambapo mara nyingi aliishia kukaa benchi huku nafasi yake akicheza Yusuph Kagoma, jambo ambalo limemfanya Kumwembe kuwa na wasiwasi.

Akiandika mawazo yake baada ya Simba kutangaza kuachana na mchezaji huyo, Edo alisema:"Hauwezi kuwa mchezaji mkali sana ukaendelea kuwa Ligi Kuu ya Nigeria. Namna ambavyo Wanigeria wanavyochomoka kila siku.

"MVP wa Nigeria kapigwa benchi na Yusuf Kagoma. Maamuzi sahihi kwa Simba. Kinachoumiza klabu ni namna ambavyo wachezaji wanaopewa Thank you walikuja klabuni miezi 12 tu iliyopita. Ina maana usajili uliopita ulivurundwa. Kuna tatizo katika scouting system ya usajili Simba,” amesema Kumwembe.

Okejepha alijiunga na Wekundu wa Msimbazi msimu uliopita akitokea Klabu ya Rivers United ya Nigeria ambako aliibuka mchezaji bora wa msimu katika ligi hiyo. Ukiachana na nyota huyo mwingine ni Nelson Okwa ambaye aliwahi kujiunga na Simba msimu wa 2023/2024 akitokea Rivers United ya Nigeria lakini hakuweza kutamba ndani ya kikosi cha Msimbazi kama ilivyokuwa kwa Okejepha.

Mbali na Okejepha wachezaji wengine waliopewa mkono wa kwaheri ni Valentin Nouma, Aishi Manula ambaye tayari amejiunga na timu yake ya zamani, Azam FC, Fabrice Ngoma na Hussein Kazi huku ikielezwa kuwa wengi zaidi wanaweza kuondoka muda wowote.