Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Droo robo fainali Uefa, iko hivi

Muktasari:

  • Mechi za hatua hiyo zinatarajiwa kupigwa Aprili 9, mwaka huu ikiwa ndiyo michuano mikubwa zaidi barani Ulaya.

Nyon, Uswisi. Droo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inapangwa leo, ambapo kila timu itafahamu inacheza na timu gani kwenye hatua hiyo.

Mechi za hatua hiyo zinatarajiwa kupigwa Aprili 9, mwaka huu ikiwa ndiyo michuano mikubwa zaidi barani Ulaya.

Hispania imeweka rekodi msimu huu ikiwa na timu tatu kwenye hatua hii muhimu, England inafuata ikiwa nazo mbili, sawa na Ujerumani Ufaransa ina timu moja kati ya nane zilizofuzu msimu huu.

Timu zilizofanikiwa kufuzu kwenye hatua hii ni Arsenal, Atlético Madrid, Barcelona, Bayern, Dortmund, Man City PSG na Real Madrid.

Kwenye michuano hii kila timu ina ubora wake na kila moja imekuwa ikipewa nafasi ya kwenda nusu fainali.


Arsenal (England)

Viwango vya Uefa: 22

Ubingwa: 0

Msimu uliopita: Ilitolewa hatua ya 16 bora Kombe la Europa.

Arsenal inapewa nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa msimu huu, kutokana na ubora wa kikosi chake, ikiwa imefuzu baada ya kuitupa nje Porto ya Ureno kwa mikwaju ya penalti

Staa: Staa wa Arsenal ni Martin Odegaard ambaye kwenye michezo ya Uefa msimu huu ameshacheza mechi saba, amefunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao.

Kocha: Mikel Arteta

Alikuwa msaidizi wa Pep Guardiola kwenye kikosi cha Man City tangu 2016 na 2019, ameshatwaa ubingwa wa FA akiwa na Arsenal kwenye msimu wake wa kwanza na kuirudisha timu kwenye Uefa, anaaminika kuwa anaweza kuifikisha nusu fainali.


Unafahamu?

Hakuna timu iliyofika hatua ya mtoano mara nyingi zaidi ya Arsenal na ikashindwa kutwaa ubingwa.


Atlético Madrid (Hispania)

Viwango cha Uefa: 13

Ubingwa:

Msimu uliopita: Ilitolewa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa

Atletico Madrid, ina uzoefu mkubwa kwenye michuano hii mikubwa barani Ulaya ikiwa imeshiriki mara kwa mara, inategemea zaidi uzoefu wa kocha, Diego Simeone.

Imeitupa nje timu mahiri ya Inter Milan ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kutinga kwenye hatua ya nusu fainali kutokana na uzoefu wake.

 Mastaa:  Alvaro Morata

Morata ameshafunga mabao matano kwenye michezo nane ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Kocha: Diego Simeone

Amekaa hapa kwa zaidi ya miaka 11, akiwa anatajwa kama kocha mwenye mafanikio makubwa akiwa Los Rojiblancos ametwaa ubingwa wa Europa mara mbili, Uefa Super Cup na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa mara mbili.


Unafahamu?

Atlético kwenye michezo 17 ya mtoano ambayo imecheza nyumbani tangu Msimu wa  1996/97, haijapoteza hata mmoja, imeshinda 10 na kutoka sare saba.


Barcelona (ESP)

Viwango vya Uefa: 12

Msimu uliopita: Ilitolewa hatua ya makundi Kombe la Europa.

Barcelona ni timu yenye wasifu mkubwa kwenye michuano hii ikiwa imeshatwaa ubingwa mara tano, ingawa nsimu huu haikuwa inapewa nafasi kubwa ya kufuzu kutokana na kiwango cha chini ambacho imekuwa ikionyesha.


Kiwango ambacho Barcelona imekionyesha nyumbani kwa kuitupa nje Napoli, kinadhiirisha ukubwa wao na kuonyesha kuwa inaweza kufanya mambo makubwa na kufuzu nusu.

Staa:  João Cancelo, huku amefanya kazi kubwa kwenye kikosi cha Barcelona hadi sasa na anaaminika anaweza kuibeba.

Kocha: Xavi Hernández

Msimu uliopita alitwaa La Liga, lakini sasa mambo hayaendi vizuri na ameshatangaza ataondoka, inawezekana akaondoka na ubingwa huu.


Unafahamu?

Barcelona ni timu ya tatu baada ya Real Madrid na Bayern kushinda michezo 200 na michuano ya Ulaya.


Bayern München (Ujerumani)

Viwango vya Uefa: 2

Msimu uliopita ilitolewa hatua ya robo fainali.

Bayern Munich ni timu nyingine yenye mafanikio makubwa Ulaya, ipo hapa ikiwa imetwaa ubingwa mara sita.

Imekuwa ikitajwa mara kwa mara kuwa inaweza kufanya makubwa kwenye michuano hii kutokana na ubora wake.

Imefika hapa baada ya kuitupa nje Lazio na leo inasubiri kujua itacheza nani kwenye robo fainali.

Staa: Harry Kane, huyu anatafuta ubingwa wake wa kwanza akiwa ameshafunga mabao sita na asisti tatu.

Kocha: Thomas Tuchel

Uzoefu wake kwenye michuano ya Ulaya akiwa aliifikisha PSG fainali vinatosha kuamini kuwa anaweza kuipa Bayern ubingwa wa saba wa Uefa.


Unafahamu?

Thomas Müller ni mchezaji wa tatu kushinda michezo 100 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Cristiano Ronaldo (115) na Iker Casillas (101).


Dortmund (Ujerumani)

Viwango vya Uefa: 11

Msimu uliopita iliondolewa hatua ya 16 bora.

Hawa ni mabingwa wa msimu wa 1996/1997, imekuwa hawafanyi vizuri kwenye ligi lakini mafanikio ya huko yanaweza kuwabeba zaidi, lakini wengi wataomba kupangwa nao leo.

Staa wa timu hiyo ni: Julian Brandt ambaye amekuwa bora kwenye kila mchezo wa timu yake msimu huu.

Kocha: Edin Terzić

Terzić, siyo kocha mwenye wasifu mkubwa lakini anaifahamu Dortmund kwa kuwa aliitumikia kuanzia akiwa na timu za vijana.


Unafahamu?

Dortmund imeshinda michezo tisa kati ya kumi ya Uefa nyumbani baada ya kutoka sare ugenini.


Man City (England)

Viwango vya Uefa: 1

Msimu uliopita: Ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga Inter Milan.

Inawezekana kila timu ikawa na hofu na Manchester City kutokana na kiwango ambacho imefanikiwa kukionyesha kwenye michezo iliyopita.

City imekuwa ikipewa nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wa Uefa kutokana na ubora wake.

Timu inawatengemea mastaa wake Erling Haaland na Julián Álvarez kufunga mabao ambapo kwa pamoja hadi sasa wamefunga 11.


Kocha: Josep Guardiola

Guardiola ni kati ya makocha wenye heshima kubwa kwenye soka duniani, alifanikiwa kutwaa ubingwa mara mbili akiwa na Barcelona na mara moja na City anatajwa kama mmoja kati ya makocha bora Ulaya.

Staa: Rodri

Huyu amekuwa mchezaji mahiri kwenye timu hii na kuiongoza kushinda michezo kadhaa ya Ulaya msimu huu.


Unafahamu?

Haaland amecheza michezo minne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora, amefunga mabao kumi.


Paris Saint-Germain (Ufaransa)

Viwango vya Uefa: 4

Msimu uliopita ilitolewa hatua ya 16 bora.


Mafanikio yao makubwa ni kufika fainali msimu wa 2019/20.

Kwa mara ya kwanza kuanzia msimu wa 2020/21, imefanikiwa kufika hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu ikiwa inataka kufanya vizuri wakati staa wake Kylian Mbappe akitarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Timu hii imekuwa ikicheza soka la kushambulia zaidi na wasiwasi mkubwa ni kwenye michezo inayocheza ugenini msimu huu.


Kocha: Luis Enrique

Kocha huyo amekuwa na ubora wa hali ya juu kwenye michezo kadhaa ambayo timu yake inacheza lakini uezoefu wake kwenye michuano ya Ulaya ukiendelea kumbeba.


Staa: Kylian Mbappé

Tayari amefunga mabao sita kwenye michuano ya msimu huu.


Unafahamu?

Mbappé amefikisha mabao 45 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa ni mchezaji wa pili mdogo kufikia idadi hiyo.


Real Madrid (Hispania)

Viwango vya Uefa: 3

Msimu uliopita ilitolewa hatua ya nusu fainali.

Hawa ni mabingwa wa kihistoria kwenye michuano hii, wakiwa wametwaa ubingwa mara 14 na sasa inatafuata mara ya 15.

Inatajwa kuwa timu bora kwenye michuano hiyo kwa kipindi chote ambapo kila ikishafika fainali inapewa nafasi ya kutwaa ubingwa.

Kila timu msimu huu haitamani kuona inapangwa na Madrid leo kutokana na ubora wake inapofika hatua hii.

Kocha:

Carlo Ancelotti ndiye kocha mwenye wasifu mkubwa zaidi kwenye michuano hii msimu huu na ameshasema timu yake inatamani kutwaa ubingwa huu.


Staa: Jude Bellingham ameifungia timu yake mabao manne akiwa pia ametoa pasi nne za mabao.

Unafahamu?

Madrid imefanikiwa kushinda michezo 37 kati ya 39 nyumbani, ikiwa imeanza kushinda ugenini.