Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Msolla ajitosa kupimana na Karia Urais TFF

Muktasari:

  • Uchaguzi Mkuu wa TFF umepangwa kufanyika Agosti 16, 2026 mkoani Tanga.

Homa ya Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeanza kupamba moto wakati leo ikiwa siku ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa Shirikisho hilo.

Taarifa kutoka ndani ya kamati ya uchaguzi zinasema tayari Rais anayetetea nafasi yake Wallace Karia ametangulia kurudisha fomu hizo jana.

Karia anatetea nafasi hiyo ya Urais akiwa ameshatangulia kuongoza vipindi viwili kwenye kuliongoza Shirikisho hilo.

Leo mgombea mwingine ambaye amerudisha fomu ni Dk. Mshindo Msolla, ambaye fomu zake zimeletwa na mwanaye Mshindo Msolla.

Akizungumza mara baada ya kurudisha fomu hizo Msolla amesema tayari baba yake ameshakamilisha kujaza fomu hizo tayari kwa kuwania nafasi hiyo.

"Nimekuja kurudisha fomu za Mzee (Mshindo Msolla) Mimi ni mwanaye, na yupo tayari kwa mchakato huu,"amesema Msolla.

Akizungumzia kuhusu uidhinishwaji Msolla amesema:"Dokta Msolla ni mwanamichezo mbobevu wa mambo ya michezo kila kitu kipo sawasawa kwake na kama mnavyoona amerudisha fomu."