Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Conte apewa miaka miwili Yanga

Muktasari:

  • Anatajwa kuwa mmoja kati ya viungo wa kisasa na ni chaguo la kocha mpya wa timu hiyo atakayetangazwa hivi karibuni.

Klabu ya Yanga imekamilisha dili la kiungo wa shoka Moussa Bala Conte  kutoka CS Sfaxien ya Tunisia kwa mkataba wa miaka miwili.

Simba ndio ilikuwa ya kwanza kumshawishi kiungo huyo wa CS Sfaxien ya Tunisia, na baadaye Yanga ikaingilia dili hilo na jana wameposti picha kwenye mtandao wao wa kijamii 'Instagram' akiwa na rais wa klabu hiyo Hersi Said na kuandika kuwa Conte ni kijani na njano.

Kiungo huyo amekuwa mchezaji wa kwanza wa Yanga kutambulishwa rasmi tangu dirisha la usajili lilipofunguliwa Julai Mosi mwaka huu akiwa anatajwa kuziba pengo la Khalid Aucho ambaye anatimka kwenye timu hiyo.

Licha ya timu hiyo kutoweka wazi kuwa wamenasa saini ya kiungo huyo kwa mkataba wa miaka mingapi Mwananchi linafahamu kuwa amesaini miaka miwili na ndiyo utaratibu ambao klabu hiyo itautumia kwa wachezaji wake wapya.

"Amesaini mkataba wa miaka miwili, dau limebaki kuwa siri ya klabu lakini kulikuwa na vita kubwa kwa kuwa Simba nao walikuwa kwenye hatua ya mwisho kabisa kumnasa, kwa kipindi hiki wachezaji wengi wageni watapewa mikataba ya miaka miwili miwili,"

Licha ya vita kubwa ya kuinasa saini ya kiungo huyo, Yanga imefanikisha dili hilo na alitua hapa nchini kuanzia juzi usiku baada ya kuruhusiwa na klabu yake ya Sfaxien kuwa akamalizane na Yanga.

Hata hivyo, habari zinasema Yanga imemalizana na Sfaxien kwa kulipa dau ambalo lilikubaliwa na Waarabu hao kisha ikapewa ruhusa ya kumalizana na mchezaji.

Kiungo huyo wa ulinzi raia wa Guinea mwenye umri wa miaka 21, alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Sfaxien unaofikia tamati 2026.

Conte alikuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Sfaxien ambapo amekuwa chaguo la kwanza la timu hiyo ya Tunisia ambayo iliishia katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025 na anakumbukwa kwenye mchezo uliopigwa hapa nchini wakati timu yake ilipovaana na Simba  kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho na kupoteza kwa mabao 2-1.

Katika msimu uliopita, Conte amecheza mechi 23 za Ligi Kuu ya Tunisia akiwa na kikosi cha Sfaxien huku akionyeshwa kadi saba za njano.

Amecheza mechi sita za Kombe la Shirikisho Afrika huku akicheza mechi mbili za Kombe la Klabu Bingwa kwa Nchi za Kiarabu.

Anatajwa kuwa mmoja kati ya viungo wa kisasa na ni chaguo la kocha mpya wa timu hiyo atakayetangazwa hivi karibuni.