Cheptegei aweka rekodi mpya Olimpiki

Muktasari:
- Ushindi huo kwa Cheptegei haukuishia kwenye medali tu bali pia Mganda huyo aliweka rekodi ya Dunia ya kukimbia kwa muda mfupi zaidi katika Mita 10,000 akıtumia muda wa dakika 26:43.14.
Ijumaa iliyopita ilikuwa siku ya furaha kwa taifa la Uganda na Afrika Mashariki kiujumla kufuatia ushindi wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 10,000 ambao mkimbiaji Joshua Cheptegei aliupata huko Ufaransa kwenye Michezo ya Olimpiki inayoendelea.
Ushindi huo kwa Cheptegei haukuishia kwenye medali tu bali pia Mganda huyo aliweka rekodi ya Dunia ya kukimbia kwa muda mfupi zaidi katika Mita 10,000 akıtu is muda wa dakika
26:43.14.
Katika mbio hizo, Berihu Aregawi wa Ethiopia akimaliza katika nafasi ya pili na kushinda medali ya shaba akitumia muda wa dakika 26:43.44 na Grant Fisher wa Marekani alishika nafasi ya tatu akitumia muda wa dakika 26:43.46.
Hiyo ni medali ya kwanza ya dhahabu kwa Cheptegei katika mashindano ya Olimpiki kwa mita 10,000 baada ya kujaribu bila kufanikiwa mwaka 2016 yalipofanyika Brazil na baadaye Japan mwaka 2020 aliposhika nafasi ya pili.
Ndoto imetimia
Muda mfupi baada ya kushinda medali hiyo ya dhahabu, Cheptegei alisema kuwa ni jambo ambalo aliweka nadhiri ya muda mrefu kulitimiza.
Anasema kuwa tangu alipokuwa kijana mdogo alitamani kushinda medali ya dhahabu katika mbio za ummalı huo kwenye Olimpiki na aliyemfanya atamani hilo ni mkimbiaji gwiji wa Ethiopia, Kenenisa Bekele.
“Kama miaka 16 iliyopita nilipokuwa namtazama gwiji Kenenisa Bekele akishinda Beijing, kilikuwa ni kitu kilichokua ndani ya moyo.
“Nilijisemea mwenyewe, siku moja, nyakati moja ninataka kuwa bingwa wa Olimpiki,” alisema Cheptegei.
Cheptegei anaamini kwamba ushindi wake utasaidia kuwaamsha vijana wa Uganda kuamini katika ndoto zao na kuzipambania ili ziwafikishe katika kilele cha mafanikio.
“Vijana wadogo mnaotazama ndani ya Uganda, mnaweza kufanikiwa. Aminini katika nyinyi kwa sababu kama hamjiamini wenyewe hamuwezi kufanikiwa katika maisha,” alisema Cheptegei.
Medali za kutosha mezani
Ushindi wa medali ya juzi unamfanya Cheptegei afikishe idadi ya medali ya 14 alizoshinda katika mashindano makubwa ya mbio ambayo ameshiriki kwa nyakati tofauti.
Katika medali hizo 14 ambazo ameshinda, Cheptegei amenyakua medali 11 za dhahabu, mbili za shaba na medali moja ya fedha.
Kabla ya kushiriki Olimpiki mwaka huu, medali ya mwisho kwa Cheptegei ilikuwa ya dhahabu ambayo alishinda katika mashindano ya dunia yaliyofanyika Budapest, Hungary mwaka jana.
Mbio za mita 10,000 ndio amezitawala zaidi kwani medali nane kati ya 14 alizoshinda zimetokana na mbio za urefu huo.
Huyu ndiye Cheptegei
Cheptegei alizaliwa Septemba 12, 1996 katika Wilaya ya Kapchorwa iliyopo mkoa wa Mashariki wa Uganda.
Wakati anaanza shule ya msingi, alipendelea kucheza mpira wa Miguu na kuruka umbali mrefu lakini alipogundua kipaji chake kipo kwingine ndipo akageukia kwenye mbio.
Mbali na kujishughulisha na riadha, Cheptegei ni msomi wa elimu ngazi ya shahada katika taaluma ya ugavi na manunuzi.
Lakini pia ni muajiriwa wa Jeshi la Polisi nchini Uganda.
Mbio zimemtajirisha
Ushindi katika mashindano tofauti ya riadha aliyoshiriki umemfanya Cheptegei kuwa miongoni mwa wanamichezo matajiri nchini Uganda.
Mwanariadha huyo anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 4 milioni, ambao amechuma kupitia fedha za zawadi za ushindi lakini pia matangazo ya biashara.