Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yatinga robo fainali Kombe la Dunia la Klabu

Muktasari:

  • Chelsea watakipiga dhidi ya Palmeiras kutoka Brazil siku ya Ijumaa mjini Philadelphia, katika mchezo wa robo fainali.

Charlotte, Marekani. Chelsea imefanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia la Klabu kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Benfica, katika mchezo uliopigwa dakika 120 uliokumbwa na mvua kubwa na radi, hali iliyopelekea mchezo huo kusimama kwa zaidi ya saa mbili.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Bank of America jijini Charlotte, North Carolina, Chelsea walipata ushindi huo kupitia mabao ya Christopher Nkunku, Pedro Neto, na Kiernan Dewsbury-Hall katika muda wa nyongeza, baada ya Angel Di Maria kuisawazishia Benfica kwa mkwaju wa penalti.

Dhoruba yazua taharuki, mchezo wasimama kwa saa mbili

Chelsea walikuwa mbele kwa bao la mpira wa adhabu kutoka kwa Reece James katika dakika ya 64, kabla mvua kubwa iliyoambatana na radi kulazimu mchezo kusimamishwa katika dakika ya 86, kwa mujibu wa taratibu za kiusalama zinazotumika Marekani.

Wachezaji waliondolewa ghafla uwanjani, jambo lililoibua sintofahamu, hasa kwa wachezaji wa Chelsea waliodai hawakuwa na taarifa za mapema kuhusu taratibu hizo. Radi yoyote inayopigwa ndani ya maili nane huzua kusimamishwa kwa dakika 30, na kila radi mpya huongeza muda huo.

Baada ya kurejea uwanjani, Benfica walitumia nafasi yao ya kwanza ipasavyo, Angel Di Maria akafunga penalti dakika ya 94 baada ya mpira kugonga mkono wa mchezaji wa Chelsea, na kufanya matokeo kuwa 1-1. Bao hilo lilikuwa la mwisho kwa Di Maria akiwa na Benfica.

Hata hivyo, matumaini ya Wareno hao yalikatizwa na kadi nyekundu ya Gianluca Prestianni aliyeonyeshwa kadi mbili za njano mfululizo dakika ya 96 na 100.

Chelsea walitumia vyema faida ya mchezaji mmoja zaidi, na katika dakika 15 za mwisho za muda wa nyongeza, walipachika mabao matatu mfululizo kutoka kwa Nkunku, Neto, na Dewsbury-Hall na kufunga pazia la mchezo huo wa aina yake.

Kocha Enzo Maresca hakuificha hofu yake kuhusu mazingira ya Marekani kuandaa mashindano makubwa kama haya, akisema hali ya hewa isiyotabirika inaweza kuhatarisha ubora wa mashindano.

Reece James na Marc Cucurella waliibuka mashujaa wa mchezo kwa kuonyesha ubora mkubwa upande wa ulinzi na mashambulizi, kiungo Moises Caicedo alipokea kadi ya pili ya njano kwenye mashindano haya, jambo linalomfanya kuukosa mchezo wa robo fainali.

Mabao mawili kati ya matatu ya Reece James mwaka huu yamepatikana kupitia mipira ya adhabu. Chelsea haikuwa imekubali shuti lolote lililolenga lango kwenye mechi mbili za awali za Kombe la Dunia la Klabu hadi penalti ya Di Maria.

Chelsea sasa watakipiga dhidi ya Palmeiras kutoka Brazil siku ya Ijumaa mjini Philadelphia, mchezo ambao unatarajiwa kuwa mgumu zaidi.