Prime
Chama anavyosubiri kauli ya mwisho Yanga

Muktasari:
- Ishu Iko hivi; ukiacha historia ya ubora wa kiungo huyo katika maisha yake ya soka hapa nchini tangu akiwa Simba, lakini msimu huu namba zake hazimbebi sana huku akishindwa ushindani wa nafasi dhidi ya viungo wenzake kwenye kikosi cha Yanga.
Hatma ya kiungo Clatous Chama ndani ya Yanga bado inapasua kichwa baada ya mabosi wa timu hiyo kusubiri uamuzi wa kocha wao Miloud Hamdi ambaye anataka kumsoma zaidi kabla ya kutoa kauli ya mwisho juu yake.
Ishu Iko hivi; ukiacha historia ya ubora wa kiungo huyo katika maisha yake ya soka hapa nchini tangu akiwa Simba, lakini msimu huu namba zake hazimbebi sana huku akishindwa ushindani wa nafasi dhidi ya viungo wenzake kwenye kikosi cha Yanga.
Chama ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja Yanga mwanzoni mwa msimu huu akichukua Dola 150,000 (takriban Sh396.9 milioni), mabosi wa Yanga wanataka endapo kocha wao atasema abaki basi watamtaka apunguze dau lake ili aendelee kujitafuta.
Msimu huu Chama amefunga mabao matatu pekee kwenye ligi lakini utata ni namna anavyoonekana kupata shida kuzoea falsafa za kikosi hicho.
“Kuna mambo mengi ya kujiridhisha kabla ya kuchukua uamuzi wa mwisho kama tumbakishe au tumuache, kila mmoja anajua ubora wa Chama lakini ndani ya msimu huu kile ambacho tulikitarajia hatujakipata sawasawa,” alisema bosi huyo wa juu ndani ya Yanga.
“Kwahiyo tumekwama hapo ukitazama gharama ambazo tulizitumia ni kubwa na sio kwamba hapati nafasi kuna mechi anazipata lakini bado unamuona haonyeshi kile kikubwa tunachosubiri.
“Tumemuomba kocha (Hamdi) naye atusaidie kupima nafasi yake, ametuambia atamuangalia zaidi kwenye mechi zilizosalia, tunataka pia aangalie nafasi yake dhidi ya viungo wengine kwa kuwa yeye ndio mtu anayejua atamtumia nani na wakati gani.
“Kama kocha atasema abaki tunaweza kumuongezea mkataba lakini tunafikiria apunguze dau lake kwanza unajua tulimchukua kwa gharama kubwa tukiamini kwamba kuna kitu kikubwa ataongeza.”